Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa nafasi hii na nikupongeze wewe pia kwa namna ambavyo unaendesha Bunge letu. Nami niseme machache kuhusu suala hili na ninaunga mkono hoja za Kamati zote mbili.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika maeneo ambayo hatujampa Mheshimiwa Rais wetu pongezi za kutosha ni kwenye kuendeleza na kuimarisha social safeness ambazo ndizo zinaenda sambamba na kuimarisha ustawi na maendeleo ya jamii yetu, ninaamini kwamba wote tunapoenda kwenye majimbo yetu kuomba mitano tena cha kusema zaidi ni hicho tu kwamba je, tumeimarisha ustawi wa jamii, je, jamii ina furaha zaidi mwaka huu kuliko mwaka 2020 au namna gani?
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kusema kweli kwenye hilo ameonesha na nataka nijiunge na wenzangu kumpongeza sana kwa kupata hiyo tuzo ambayo anapokea siku ya leo ya kuweza kupunguza vifo vya watoto kutoka 556 hadi 104, ni haki yake kabisa apokee. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, njia moja ya kuhakikisha kwamba wananchi wengi au kila mwananchi anashiriki kwenye mafanikio nchi hii inayopata kwenye kukuza uchumi wetu ni hili la kwamba kuna vitu, kuna huduma za jamii, kuna vitu ambavyo vinafanyika kwenye jamii ambavyo mwananchi halipii kama ambavyo ingetakiwa kama ingekuwa tu ni soko huria. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa njia moja ni hii ya kuongeza na kupanua upatikanaji wa huduma za jamii kama vile afya, elimu, maji, umeme pamoja na usafiri ambao ni rahisi unaweza kufikisha mazao kwenye masoko na kwa bei nafuu, pamoja na kuhakikisha kwamba vituo vya afya, kwa upande wa vituo vya afya vipo karibu na majumba yetu na pale tunapoishi ili kwamba mwananchi asitumie gharama kubwa katika kupata hiyo huduma na mambo mengine mengi ambayo wote tunashuhudia kwamba yamefanyika kwa ufanisi sana wakati huu wa Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninasema kwamba income distribution ni somo humu sana kwenye uchumi kwa sababu watu hawajui wafanye nini, mara nyingi tunaambiwa kwamba pato limekua watu hawana fedha, fedha haionekani mifukoni.
Mheshimiwa Naibu Spika, niliwahi kusema hapa kwamba fedha iliyopo mfukoni siyo ya thamani kama ile ambayo unapata bure, mtu ameshakutengenezea kupata elimu bure, matibabu bure, kupata matibabu ambayo zamani ungeyafuata kwenye nchi nyingine, lakini sasa unayapata hapa kwa bei nafuu au mara nyingine hata bure na unaweza ukasamehewa kama hujiwezi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kwa maana ile tunasema kwamba kila mtu kwa namna moja anashiriki kwenye mafanikio ya nchi yetu na naamini kwamba siyo suala tu la miundombinu, lakini ni hili la huduma za jamii ambalo naamini kwamba wenzetu wa Kamati inahusika wamelizungumza kwa ufanisi na wametoa maazimio ambayo yanakubalika sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kwamba pale kwenye jimbo langu tulipokuwa tunaingia kwenye Bunge huku mwaka ule 2020 tulikuwa na sera inayosema kwamba kila kata itapata kituo cha afya. Sasa tatizo moja ni kwamba tulivyoingia tukaeleza vizuri na tukakubali siyo tu kwamba upewe kwa sababu ni Kata, tuangalie uhitaji na kweli hiyo sera ya usawa kwenye kugawa huduma za jamii na vitu vingine ikiwa ni pamoja na ambulance, vituo vya afya na kadhalika.
Mheshimiwa Spika, tulikubali kwa sababu ni lazima kuwe na usawa, sasa usawa unaletwa kwa namna gani? Mojawapo ya kigezo cha usawa ni kugawa kulingana na idadi ya watu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa pale kwenye Jimbo langu nina watu elfu mbili karibu na sabini elfu, wapo wanatakiwa wahudumiwe na vituo vitatu tu vya afya. Sasa ukiniambia kwamba hiyo ni sawa nasema usawa upo wapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tuna data na mimi nataka niombe sana Wizara inayohusika na Mtakwimu wetu Mkuu wa NBS atoe hizi data kwa ufasaha zaidi ili watu wajue kwamba ni wapi pa kupeleka kituo cha afya, kama kuna ambulance wanagawa, ni nani apewe ngapi na kwa sababu gani. Tunasema unatoa item per seven unit or population. Kwa maana ya kwamba kila watu 10,000 wapate angalau zahanati, lakini kama hiyo haipo inakuwa haijaleta tija sana kwa wale watu ambao walikuwa wanafikiri kila Kata inapata.
Mheshimiwa Naibu Spika, kusema kweli ukiangalia ukubwa wa Kata zetu naamini kwamba kila Kata na population ya sasa hivi ambayo tumepata kutoka sensa ilivyofanyika kila Kata ingestahili kupata kituo cha afya, niseme hilo ni sawa sana, nirudi kwenye issue hii ya kusema kwanza social safeness watu wanafikiria tu ni hiyo tu ya huduma lakini hata hili suala zima la uwezeshaji ambalo linazungumzwa hapa, uwezeshaji wa vijana, wazee, wanawake na wengine wote ambao wanaweza, hata na wazee kama mimiā¦ Aah, mimi siyo mzee samahani. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kwamba uwezeshaji wa watu ambao wana nguvu na uwezo wa kufanya biashara au kujiajiri. Kwa hiyo naomba kwamba hili liwekewe mkazo. Ninafikiri tumekuwa tunajaribu jaribu, watu wamekuwa wanatoa mapendekezo kwamba pengine ile mifuko ya uwezeshaji iwekwe mahali pamoja au kwenye taasisi mbili ili iweze kusimamiwa vizuri na iwekezwe, issue ya kwamba ile mifuko yenyewe inaweza ikadhamini watu, ikadhamini mabenki yakatoa fedha nyingi zaidi ili mifuko nayo ikue. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukinipa dhamana ya shilingi elfu kumi inaweza ikatoa mikopo mara kumi ya ile, lakini najua kwamba huyu mtu possibility ya ku-default haizidi 10%. Kama mtu ana possibility ya ku-default mikopo kwa asilimia zaidi ya kumi hapewi mkopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama ni hivyo, kama default rate yangu ni ten percent naweza nikakopesha mara kumi ile hela ambayo umenipa, kwa hiyo ninasema pengine tuliundie mchakato ili tuweze kufikia sera hiyo, tutengeneze sera ambayo inaeleweka vizuri kuhusiana na issue nzima ya ustawi wa jamii katika kuwasaidia watu kujiajiri na kujitengenezea kipato na wakaishi kwa furaha zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niishie hapo, lakini niseme tena kwamba nawapongeza wote na kwa vile kesho sitopata nafasi ya kuhutubia basi ninawapongeze wana-CCM wote kwa kutimiza miaka 48 wanayoadhimisha kesho, ahsante sana. (Makofi)