Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 Na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Eng. Dr. Leonard Madaraka Chamuriho

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 Na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

MHE. ENG. DKT. LEONARD M. CHAMURIHO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia katika hoja hizi ambazo zimewasilishwa na Wenyeviti wawili. Kwanza napenda kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kutuongoza vizuri kwa kutekeleza vizuri falsafa zake nne za 4R kwa kusisitiza Utawala Bora wa Sheria, sifa ambazo zimemfanya achaguliwe tena kuwa mgombea pekee wa Chama chetu cha Mapinduzi, na sifa ambazo zinamfanya apate tuzo mbalimbali za Kimataifa, kama aliyoipata jana. Kwa hiyo, tunampongeza sana kwa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napenda kuwapongeza Wenyeviti wote wawili kwa uwasilisho wao mzuri wa hoja zilizotolewa. Vilevile napenda kuwapongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuratibu Wizara zote kuja kuwasilisha katika Kamati yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu ambalo Bunge limepewa katika Ibara ya 64 (1) ya Katiba la Kutunga Sheria na Kuzisimamia pamoja na ile ya kumkabidhi mtu yeyote kufanya shughuli hiyo, Ibara 97 (5), lazima tulilinde kwa wivu mkubwa. Hivyo, hizi dosari mbalimbali ambazo tunaziona ni lazima zirekebishwe ili tuendane vizuri na kusudio la Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitachangia majedwali yaliyowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Sita na Kumi na Saba na ningependa kutoa mifano ifuatayo ya dosari hizo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Tangazo la Serikali Na. 264 ambalo Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru, Halmashauri ya Biharamulo. Jedwali la Nne limetoza ushuru kwa wanyama wachache kuliko wale ambao wanapatikana katika masoko yetu. Hiyo inaweza kusababisha halmashauri hiyo kukosa ushuru na ikapingana na lengo la sheria mama.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ukiangalia katika Sehemu C ya jedwali hilo hilo, utakuta kuna mazao ya misitu ambayo yametoza ushuru wa milango, madirisha, fito na kadhalika, lakini hawakusema kama wanatoza kwa mlango mmoja, milango yote au kadhaa. Hivyo, hiyo inaleta sintofahamu kwa kutoweka kipimo, na italeta utashi kwa watekelezaji ambao wanaweza wakapotosha lengo jema la sheria iliyotungwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia Tangazo la Serikali Na. 510 ambazo ni Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Simanjiro na vilevile ukiangalia jedwali lake la kwanza kipengele cha Sita, kuna Ada ya Wakandarasi imesema kwa kila cheti inatoa asilimia mbili. Sasa unajiuliza, hii asilimia mbili kwenye kila cheti cha mkandarasi ni nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maoni yangu, hii italeta mkanganyiko kwa sababu, siyo kodi inayotozwa kwenye Certificate ya Mkandarasi, bali walikuwa wana maana ya kitu kingine kabisa, appreciations certificates. Kwa hiyo, Kamati imewaelekeza wakalibadili hilo liende vizuri, ili hawa wakandarasi wetu wasipate changamoto katika utekelezaji wao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tukiangalia katika ada na ushuru wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Kifungu cha 15, Namba mbili, kimeweka utaratibu wa kuuza bidhaa ambazo zimekamatwa na Halmashauri, lakini Kifungu hicho hicho kiko kimya kuhusu hela za ziada ambazo zitabaki. Kwa hiyo, tumewaelekeza kwamba, ukikamata bidhaa ukaiuza, utakavyorudisha ile fedha, chenji ni lazima umrudishie mwenyewe na haiwezi ikabaki kwa halmashauri tajwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna jedwali la kwanza Sehemu J, ambayo haina uhalisia katika utozaji wa CSSR ambayo wamepanga kwamba, wanatoza Ushuru wa CSSR wa shilingi 100/= tu kwa kilo moja ya dhahabu. Sasa ukiangalia thamani ya dhahabu kilo moja na kutoza ushuru wa shilingi 100/=, unaona hii hapa ni lazima kuna kosa katika uandishi wa hilo jedwali. Hivyo tumesema likabadilishwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Chunya hiyo hiyo, jedwali hilo hilo la kwanza, kipengele cha kwanza, cha nne na cha tano, wametoza ushuru wa mazao kwa asilimia tatu, lakini hawakusema hii asilimia tatu ni ya kitu gani? Hivyo, tumewashauri waende wakabadilishe ili kuweza kuweka mizania sawa. Kwamba anayetoza ushuru aweze kuelewa ni kitu gani hasa ambacho anaweza akatakiwa kutoza huo ushuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakiniā€¦

(Hapa kengele iliashirikia kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante Doctor.

MHE. ENG. DKT. LEONARD M. CHAMURIHO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)