Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 Na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 Na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue fursa hii kumshukuru Mungu, kwa kuwa ametujalia kukutana hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nichukue fursa hii kukushukuru wewe, Wajumbe wa Kamati hii ya Utawala, Katiba, na Sheria pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote kwa namna ambavyo wametoa michango yao ambayo kwa kweli iko very constructive; na inaonesha wazi kwamba wametoa michango hii wakiwa wana mustakabali mwema wa kulijenga Taifa hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nichukue fursa hii kumshukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Dkt. Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa wanayoifanya, hasa katika kusimamia, kulinda, kuendeleza, na hatimaye Muungano huu keshokutwa unakwenda kutimiza miaka 61. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi nyingi sana duniani zilijaribu kutaka kuungana, lakini zilishindwa na ziliishia njiani. Leo nchi yetu inakwenda kutimiza miaka 61 ya Muungano huu. Ni kazi kubwa iliyofanywa na viongozi wetu kwa sababu ya busara ya viongozi wetu wa pande zote mbili; Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Dkt. Mwinyi wana busara ya hali ya juu katika kuulinda na kuuendeleza Muungano huu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uwepo wa Kamati ya pamoja inayoshughulikia mambo yote ya Muungano, na kuhakikisha kwamba panapotokezea jambo linaloleta mgongano, Kamati hii inakutana kwa kushirikiana pande zote mbili. Lengo ni kuhakikisha kwamba muungano huu unaendelea kubaka salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kubwa zaidi ni dhamira ya viongozi tulionao. Watanzania bado wana nia na dhamira ya kuuendeleza Muungano huu. Maana yake ni kazi kubwa inayofanywa na viongozi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa kumekuja hoja, ama moja miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa, ni jambo la uwepo wa Ofisi za Muungano. Kwanza uwepo wa Ofisi ya Makamu wa Rais inayosimamia Muungano kwa upande wa Zanzibar, na pia uwepo wa ofisi za kudumu kwa baadhi ya ofisi kupitia Wizara ambazo zina nasaba na Muungano kwa upande wa Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, na Watanzania kwa ujumla kwamba, zipo taasisi 33. Zote hizi ni taasisi ambazo zinagusa kwenye Muungano, na kati ya hizo, 21 tayari zimeshakuwa na majengo yao yenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kikubwa zaidi, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge kwamba, tayari Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano tumeshaanza mchakato wa kutafuta ofisi itakayokuwa ndiyo ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa upande wa Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kubwa lingine nataka niwaambie tena Waheshimiwa, Mheshimiwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa. Ndani ya kipindi chake, zaidi ya changamoto 15 zimepatiwa ufumbuzi kwa lengo la kuhakikisha kwamba Muungano huu unaendelea na unadumu. Nawaomba Watanzania watambue kuwa, Muungano wetu ndio Utaifa wetu. Tuendelee kuuenzi Muungano wetu kwa ajili ya maslahi mapana ya vizazi vinavyokuja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kupokea taarifa hii, lakini tuwaambie tu Waheshimiwa Wabunge, yote waliyoyaelekeza na waliyoyachangia pamoja na Kamati, tunakwenda kuyafanyia kazi, ahsante. (Makofi)