Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Ummy Hamisi Nderiananga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA): Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Nianze kwa kuipongeza Kamati ya PAC. Nampongeza Mheshimiwa Mwenyekiti, Mama Kaboyoka, Makamu wake Mheshimiwa Hasunga na Wajumbe wote wa Kamati. Tunawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, binafsi nimesikiliza michango ya Waheshimiwa Wabunge na nimepitia Taarifa ya Kamati kwa kina, tunawashukuru sana kwa namna ambavyo wameendelea kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Serikali, chini ya Waziri wangu, Mheshimiwa William Lukuvi, tunapokea maazimio yote ya Kamati hii na tunawahakikishia kuwa, Wizara zote za kisekta zitaenda kuyafanyia kazi, ahsanteni sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)