Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa muda kidogo wa kuhitimisha hoja ya Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Waheshimiwa Wabunge wote waliotoa michango yao kwa hoja hii muhimu inayohusu uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma. Michango yao imetolewa kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu, na kwa vile kuna kipindi cha uchaguzi kinafuata, nimeelewa mengine ambayo labda hayakuwekewa msisitizo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, Waheshimiwa Wabunge waliochangia wengi ni wa Kamati yangu, sikuona mwingine wa nje, isipokuwa Mheshimiwa Naibu Waziri, Ummy; na kwa kuwa, hakuna yeyote aliyepinga hoja nilizozitoa, naomba tu nisisitize kwamba, yale maazimio yote niliyokuwa nimeyatoa ambayo yako pia kwenye taarifa yetu, yote yaingie katika Hansard. Pia majina yote ya Waheshimiwa Wabunge, Wanakamati wa Kamati ya PAC, yaingie kwenye Hansard.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba Bunge sasa lipokee Mapendekezo yote ya Taarifa ya Kamati kuhusu Shughuli za Kamati kwa Kipindi cha Kuanzia Februari, 2024 hadi Januari, 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)