Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Jang'ombe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Awali ya yote, tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametupatia uhai na leo kufika hapa, kuja kuangalia maslahi ya nchi yetu, kupanga maendeleo na pia, kuweka sawa ustawi wa wananchi wa Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi waliozungumza walikuwa wanataja maendeleo ya vitu. Vingi vilivyotajwa hapa ni vitu, lakini kuna maendeleo mengine inawezekana ikawa, pengine huwezi kuyaona kwa kuyashika, siyo tangible kwa sababu, huwezi ukaya-count kama ambavyo una-count barabara, kama unavyo-count visima au unavyo-count vijiji. Tumeahidi kwa wananchi kwamba, tutaweka ustawi au tutatizama maendeleo ya watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu nilichokusudia kuzungumza hapa ni maendeleo ya watu. Nakwenda moja kwa moja katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 8(a) inasema kwamba: -
(a) Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na Serikali itapata madaraka na mamlaka yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii; na
(b) Lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi nipo katika Kamati ya Ustawi wa Jamii. Sisi pale tunashughulika na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo mifuko hiyo ndiyo inatoa ustawi kwa watu ambao wapo katika shughuli zao za kazi, pengine watapata majanga watakuwa wanapata compensation, lakini pia, uzeeni watakuwa wanategemea kupata matibabu na vitu vingine kama tunavyojua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, majukumu makubwa ya hii mifuko yetu ambayo tumeipa, moja, ni kufanya uandikishaji wa wanachama ambao ni wafanyakazi, na sasa hivi tume-extend madirisha, tunakwenda mpaka kwa watu binafsi waliojiajiri wenyewe. Pia, kupokea michango kwa wanachama, kufanya uwekezaji kwa ajili ya kutunza hizi fedha zisije zikaathirika na mambo ya mfumuko wa bei, na pia, kulipa mafao kwa wanachama. Ni maendeleo makubwa ambayo yamepatikana katika hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kwa kila kipengele. Tunaishukuru na kuipongeza sana Serikali kwa kuisimamia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, nianze na Mfuko wa NSSSF. Kwenye NSSSF pale ukiangalia idadi ya wanachama ambao ndio wanashughulikiwa hapa katika kuandikishwa imeongezeka na hata uchangiaji nao umeongezeka. Ukija katika PSSSF vilevile, ukija WCF unakuta vilevile. Kwa hiyo, unakuta huduma hizi zimeboreshwa, zimeongezeka. Ukitazama katika uandikishaji na uchangiaji wa wanachama katika huu mfuko umeboreka na kuwa vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inatoa indicator gani? Ni indicator kwamba, watu wanapokwenda kustaafu, bado wataendelea kupata uhakika wa maisha yao ya kila siku ambayo yanaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna changamoto katika uandikishaji na kupeleka michango. Changamoto moja ni usahihi wa taarifa za wanachama, na nyingine ni ucheleweshwaji wa michango. Hizi taasisi zetu zimeanzisha mifumo ambayo inaenda vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nishauri kwamba, kwa kuwa garbage in, garbage out, utakachokitia katika mfumo ndicho kitakachokuja kutoka, kama jawabu katika huo mfumo, kwa maana hiyo, nilikuwa nasema kwamba, hii mifumo ambayo imeanzishwa, ni lazima iendane au isomane na ile mifumo katika ajira au katika utumishi, na hapa ndipo tutakapohakikisha hizi taarifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni usahihi huu wa taarifa utatokana na Serikali. Kwa hiyo, hapa naiomba Serikali katika kubadilisha wale wafanyakazi wanapobadilishwa madaraja yao ya mshahara na wanavyobadilishwa vyeo, kwa sababu, inakuja changamoto kama mtu hajabadilishiwa mshahara wake, amepanda cheo halafu ikafika siku ya kustaafu bado mshahara siyo sahihi, au mchango sahihi haukupelekwa. Hapa huyu mfanyakazi ndiyo hizi lawama zinazokuja. Pamoja na pongezi hizo tulifanyie kazi hili jambo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ni hawa watu wanatunza fedha. Mimi hapa nimejaribu kufanya calculation nyingi, kutokana na muda siwezi kuzisoma zote, lakini ukitazama kwamba, mifuko ina uwezo wa kulipa kwa mwaka three times kutokana na zile rasilimali ambazo wanazo, walizokusanya na mapato kutokana na uwekezaji, kwa sababu, makusanyo ya michango yameongezeka, nizungumze kwa ujumla ule uwekezaji. Mapato kutokana na uwekezaji, umeongezeka ambapo ukiweka mapato ukigawa kwa mafao ambayo yanatarajiwa kulipwa, utakuja kuona kwamba, mifuko ina uwezo wa kulipa more than three times.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaipongeza sana Serikali, Mheshimiwa Waziri Mkuu katika hili hongera sana kwa sababu, kilikuwa ni kilio cha watu. Sasa hivi mtu ana uwezo wa kulipwa hata kama ni ndani ya miezi miwili baada ya kustaafu. Sasa hivi sisi Wabunge tunachelewa kupokea mishahara kuliko wastaafu wanavyopata pensheni, wao kabla ya tarehe 25 ya kila mwezi wanakuwa tayari wameshapata na wanashughulikiwa kila kitu chao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kitu kimoja, kwenye uwekezaji, hii mifuko wametupatia comfort kubwa sana kwa maana ukitazama wao wamesema wanajilinda na rate inflation. Sasa hizi fedha ziko juu, yaani income own investment iko juu mara mbili zaidi kuliko ile inflation ya katika nchi. Sasa hapa naomba tuipongeze Serikali na pia, tuendelee kushika uzi huo huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri hapa ni kila tutakapowekeza, basi tujaribu kutazama kuwekeza kwenye tija zaidi. Hatusemi kwamba hii haijawekezwa kwenye tija, tuwekeze kwenye tija zaidi. Tujaribu kutazama maeneo ambayo tutapata multiply effect ili tuweze kuboresha pia maisha ya wananchi wengine ambao labda sio wanachama wa hii mifuko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nije katika kitu kimoja ambacho kila mwaka hapa lazima nisimame nizungumze, ni kuhusu SDL. Kuna makubaliano kuhusu hii Skills Development Levy baina ya Serikali na sekta binafsi, kwamba one third itakwenda kutizama gap of skills ambazo hizi kampuni zinazochangia ndizo zinazotoa hizo fedha ili ile skill ije kwa wananchi, ili hawa watu wasiende kuwaajiri watu wengine wa kutoka nje. Leo tunafurahi kupokea fedha kwa sababu ya kutoa vibali vya ajira, kumbe ile kazi ingeweza kufanyiwa hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu wa ATE wanasikitika, na masikitiko yao kwamba wao ndio wanaomlisha ng’ombe majani, ila maziwa yanakamwa na mtu mwingine, sasa wao hawafaidiki na michango hii. Ukitizama hapa; nitaikabidhi trendy ya michango ya SDL na ile one third inayotakiwa ambayo hata hivyo haifiki; hata moja ya kumi na tano ambayo ndiyo inayokwenda katika kutizama gap of skills ambayo Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ndiyo inayoshughulikia. Hili lingefanyika katika uratibu mzuri, lingekuja vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo hapa kwamba tunatoa vibali, tunapokea fedha, lakini tunanyima ajira za Watanzania wenzetu. Leo ukiingia mtaani utakuta hata kidampa kinaendeshwa na Mchina. Hivi hapa imeshindikana kupatikana mtu wa kuendesha hiki kidampa! Kwa hiyo, hii ni lazima tutazame.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, tumetoa kazi kwa watu ambao wamesema watarithisha ujuzi lakini ule ujuzi hawarithishi. Anafika mtu anamaliza mkataba wake, amesema baada ya miaka mitatu ataacha ujuzi lakini hakuna ujuzi ulioachwa. Kwa hiyo, tunawaacha Watanzania wenzetu hawana ajira ndani ya nchi yao na ajira zinachukuliwa na wageni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sipendi kutaja taasisi ambazo zimeingia mikataba, lakini zipo taasisi zina mikataba. Hii mikataba ya kuacha ujuzi kwa wananchi, ingekuwa zinaratiwa pia na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa sababu ndiyo inayosimamia masuala ya ujuzi. Huku kwingine ni sawa, Wizara ya Fedha watakuwa na mkataba, na vendor atakuwa na mkataba, Wizara ya Kilimo na mtu mwingine, lakini hakuna taasisi inayoweza kwenda kuratibu ndani ya Wizara ya mwenzake. Kama hawakufanya hivyo, na kama hawajafahamiana, tutakosa ajira nyingi za Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumze jambo moja ingawa wenzangu wengi wamezungumza. Unajua kuna watu wengine ni majuha. Juha sifa yake kama hukumtaja, juha anakuwa havumi; lakini juha kila ukimtaja, yule huja anapata kichwa. Kwa hiyo, na sisi lipo juha humu tunalitajataja, kwa nini tusiliachie? Yule mtu tayari ameshapata mahana, na watu wameshamtoa maana. Baada ya kumahanika, amekuwa hana maana; hamwoni kwamba hata wananchi wameshamjua kwenye mikutano yake hawaendi!
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kama ningelikuwa nasikilizwa na Waheshimiwa Wabunge wenzangu, juha hili tungeliacha kwa sababu hili juha ukilitaja linapata kichwa. Tunampa milage ya bure. Ya nini mtu kama yule? Mtu ana laana mpaka ya Baba wa Taifa, kwa sababu anasema hii nchi haijakombolewa, yeye ndio anatafuta ukombozi. Wale wazee wetu walifanya nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu Msajili wa Vyama vya Siasa tunapitisha bajeti yake hapa, kuna juha huyo anasema nchi haijakombolewa. Hatuna ajenga katika nchi hii za kuzungumza! Hivi kweli kipo chama kinaweza kikaundwa hapa kikawa ni chama cha ukombozi! Kwa hiyo, tulikuwa tunataka tutazame mambo haya kwa sababu watu hawa tayari wameshaingiwa na mahana, lakini sasa na wananchi wameshawatoa maana kwa sababu wamehamanika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, naunga mkono hoja mia kwa mia. (Makofi