Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Amina Daud Hassan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. AMINA DAUD HASSAN: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kutuletea hotuba ya mwaka wa fedha 2025/2026 ambayo imesheheni mambo ya maendeleo katika nchi. Pia niwapongeze watendaji wako wote kwa utendaji wao wa ufanisi na waliokupa ushirikiano mema pia Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko pamoja na viongozi wote wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, ninampongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri tangu alipoanza kuiongoza nchi hii tarehe 19 Machi, 2021. Nimpongeze pia kwa sababu kumekuwa na mafanikio makubwa aliyoyapata katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020. Kwa kweli ametekeleza kwa vitendo na matokeo yanaonekana na vilevile katika kipindi cha uongozi wake tumeshuhudia mafanikio makubwa katika kila kona ikiwemo kuimarisha miundombinu, kuboresha utoaji wa huduma za kiuchumi na jamii, kusimamia utawala bora, kuongoza mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi na kuhamasisha uwekezaji, diplomasia ya kiuchumi na ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Muungano wetu, Serikali inaendelea kuratibu vikao vya Kamati ya Pamoja kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi kwa ajili ya kushughulikia masuala ya Muungano. Katika mwaka 2024/2025 vikao viwili vya kujadili masuala ya Muungano vilifanyika na kupitia vikao hivyo ilifanyika tathmini ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Pamoja ya kushughulikia masuala ya Muungano. Kutokana na vikao hivi wananchi wa pande zote mbili wamenufaika kwa makubaliano yaliyowekwa kwa maslahi ya pande zote za Muungano.

Mheshimiwa Spika, mirada mbalimbali ya kimaendeleo inatokana na maendeleo ya Muungano wetu. Tukiangalia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III); miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji ya Bahari ya Hindi, Sipwese Pemba na mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika pamoja na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kama ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, mirada ya programu za kukuza uchumi, kupunguza umaskini na kuboresha maisha; miradi hii imeleta mafanikio makubwa kwa wananchi kwa kutatua changamoto mbalimbali hasa katika kaya maskini kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, pia nizungumzie ushuru wa forodha kati ya pande mbili ya Muungano; naishukuru sana Serikali yangu ya Jamhuri ya Muungano kwa kuweka bayana ushuru wa bidhaa zote ambazo zimeainishwa katika bango maalumu katika pande zote mbili za Muungano kwenye maeneo ya Bandari ya Zanzibar pamoja na Bandari ya Der es Salaam, lakini bado kuna ukosefu wa viashiria vya uadilifu kwa wananchi hasa kwa wanaohama katika pande za Muungano.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali yetu izidishe nguvu katika suala hili kwani inaharibu taswira ya Muungano wetu.

Mheshimiwa Spika, hivyo namba kuunga mkono hoja, ahsante.