Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoifanya na wewe Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kusimamia vyema shughuli za Serikali kwa umakini, kwa kujitolea na kizalendo. Kwa ufuatiliaji na utendaji wako imesaidia kuwabaini watendaji wasiosimamia vyema miradi ya Serikali ipasavyo.
Mheshimiwa Spika, katika mchango wangu nitajikita katika maeneo matatu ya kilimo, maji na miundombinu ya nishati na maji.
Moja ni kuhusu kilimo, ninaipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa pembejeo za zao la korosho bure kwa wakulima. Hii imesaidia kuongezeka kwa mikorosho inayohudumiwa na hiyo kuongeza uzalishaji wa zao la korosho kutoka tani 244,000 hadi tani 500,000 kwa msimu uliopita. Ushauri wangu ni kuiomba Serikali kuendelea kutoa pembejeo ya ruzuku na kutatua changamoto zilizopo kwenye tasnia ya korosho baadhi yake ni tozo nyingi, upungufu wa maghala na kadhalika.
Pili, naishukuru Serikali kwa maboresho na upanuzi wa mradi mkubwa wa maji wa Makonde, kwa sasa mradi huu unasuasua kwa sababu mkandarasi anadai fedha. Naomba mkandarasi alipwe ili aweze kuendelea na utekelezaji wa mradi.
Tatu, Barabara ya Kibiti - Lindi imeharibika na inahitaji ujenzi upya na si ukarabati. Naomba ujenzi wake uzingatie mahitaji halisi ya barabara hiyo. Aidha, miundombinu ya nishati kwa Mikoa ya Kusini iimarishwe ili ipunguze kukatikakatika kwa maji.