Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. BAHATI KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ametufanyia Watanzania.
Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia kwa ufupi kama ifuatavyo nikianza na mafanikio makubwa ambayo tumeyapata katika sekta zote, nani kama Samia? Niwaombe Watanzania wote wasisikilize matapeli wa kisiasa, tulikuwa na shida ya usafiri kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma, leo tunatumia saa chache tu tumefika Dodoma.
Mheshimiwa Spika, lililobaki kwa sasa tuangalie usafiri wa majini kwa zile sehemu ambazo hawajapata usafiri wa marine.
Mheshimiwa Spika, tuipongeze Serikali kwa kupata umeme na pia tubadilishe miundombinu ili wananchi waweze kufanya biashara zao vizuri.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.