Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tandahimba
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, lakini kipekee kabisa nimpongeze sana Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa sababu ameleta tafsiri sahihi ya kumtua mama ndoo kichwani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ningepewa nafasi ya kuchagua Mawaziri watatu bora katika Bunge hili, basi Mheshimiwa Jumaa Aweso angekuwa miongoni mwao, na amejaribu kuheshimisha vijana kwa kuonesha uwezo wao. Mheshimiwa Rais kama itampendeza, ninaamini anakwenda kushinda Ubunge kule Pangani, abaki hapa ili aendelee kutekeleza matakwa ya Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi watu wa Mtwara hususani Newala, Tandahimba na Nanyamba ni watu ambao tumepata shida ya maji kwa muda mrefu na tumekuwa na Mradi wa Maji wa Makonde ambao takribani tangu tumepata uhuru haukuwahi kutengewa japo shilingi bilioni moja. Lakini kwa dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais ule mradi leo tunavyozungumza wakandarasi wako site na ametoa fedha shilingi bilioni 84.7. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwangu Tandahimba, katika mambo ambayo tunafikiria kuyafanya sisi Wamakonde kuna lugha tunaita kumbamba ndija yaani kitu kinajaa halafu unaongeza kujazia. Kwa yaliyofanywa sekta ya maji na Rais Samia kupitia Jumaa Aweso hatuna sababu ya mwaka 2025 kupoteza kura hata moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunayo miradi ya maji ambayo ilikuwa imesuasua kwa muda mrefu. Tuna Mradi wa Maji wa Mkwiti ambao leo tunavyozungumza mkandarasi ameshalipwa fedha na kilichobaki sasa ni kumaliza vioski vidogo ili maji yaanze kutoka, na kwenye hili Mheshimiwa Aweso kuna kamgogoro kadogo ambacho ninakuomba sana wakati unafanya hitimisho uone namna unavyoweza kuliweka hili jambo sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo deni la milioni nne la watu wa Makonde kuwadai watu wa RUWASA. Kumbuka ule mradi bado mkandarasi hajaukabidhi kwa wananchi na wakati anafanya testing ilikuwa ni lazima wananchi wayaone maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kumekuwa na shida maji hayajazwi pale kwenye tenki, kwa sababu watu wa Makonde wanadai RUWASA shilingi milioni nne. Kwa hekima zako na busara zako ninaamini tukishahitimisha hii bajeti, kwa maana tunakwenda kuipitisha ili jambo Wizara mlichukue na mlimalize. Mmetoka kutoa taarifa hapa kwamba Mheshimiwa Rais anayafuta madeni ya maji, basi pamoja na hayo madeni hili unaliweza Mheshimiwa Aweso. Nione unalichukua kama wewe na hili jambo liishe ile wale watu wa Mangombyam wale watu wa Nanjangam wale watu wa Ngunjam wale watu wa Namindondim wale watu la Mkwitim wale watu wa Likolombe na wale watu wa Kidoo, waweze kupata maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mradi ambao Mheshimiwa Waziri atusaidie. Mradi wa Maji wa Mtopwa – Orodaleo. Ule mradi uko kwenye michakato yenu, sasa niombe muinasue kwa sababu wananchi wanaufahamu vizuri na ni mradi mkubwa wenye thamani zaidi ya shilingi bilioni tisa, ambao kama mtaufanya uende kwa haraka unakwenda kutupatia matumaini na maongezeo ya kura za Mheshimiwa Rais kwenye uchaguzi huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mradi huu wa maji tunaozungumza wa Makonde mkandarasi amesha-raise certificate anahitaji shilingi bilioni 3.1 aweze kuendelea na kazi na ule mradi unalisha Newala, unalisha Tandahimba, unalisha na Nanyamba muone namna mnavyoweza ku-fast track na wenzetu wa Wizara ya Fedha ili mkandarasi huyu alipwe fedha mambo yaweze kukimbia.
Mheshimiwa Waziri, tunao mradi ule pia wa Nanyuila – Maundo mkandarasi nae ame-raise certificate bado hajalipwa na mradi ule pia unaenda kuhudumia kata zaidi ya tano, Kata ya Lukokoda, Kata ya Kwa Nyama, Kata ya Maundo, Kata ya Mchichira na Kata ya Mnyawa. Niwaombe sana muone namna mnavyoweza kukimbizana na haya ma-certificates ili waweze kulipwa wananchi wale wanataka matokeo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na bahati njema Mheshimiwa Aweso hii umeliweza kwa Tandahimba leo ukienda ilivyo Kitama watu wanapata maji kwenye vijiji vyao, ukienda Mkundi watu watapata maji kwenye vijiji vyao, hata visima hivi ulivyovichimba vitano mmefanya kazi kubwa kwenda kuweka na solar panels watu wanapata maji. Niwaombe sana, sana, sana pelekeni fedha ili wakandarasi wamalize miradi ile ili wananchi wetu waweze kupata maji safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)