Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia katika Wizara hii muhimu sana ya maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika nchi yetu na hasa katika Wizara hii ya Maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso kwa namna ya pekee anavyopambana katika mikoa yetu na majimbo kuhakikisha wananchi wanapata maji katika kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan hongera sana Mheshimiwa Jumaa Aweso, wewe na Naibu Waziri wako lakini na watendaji wote wa Wizara ya Maji akiwemo dada yetu Ndugu Mwajuma hongera sana, hongereni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema hivyo nikiwa namaanisha Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameibeba ajenda ya kumtua mwanamke ndoo na hata sisi tunaotokea katika Kanda ya Ziwa ameibeba ajenda hiyo kupitia Ziwa Victoria kuhakikisha wananchi wa Kanda ya Ziwa wanapata maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamaanisha hivyo ukienda katika Mkoa wa Mara sisi Wana-Mara tumepata miradi mikubwa na midogo. Katika miradi midogo ya maji tumepata miradi ya maji miradi 100 ambayo miradi ile imegharimu shilingi bilioni 35.77 itaenda kuhudumia wananchi 4,667 hii ni dhahiri kwamba Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatupenda sana katika ndani ya miaka minne hiyo kazi imefanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumepata miradi mikubwa ya maji, tumepata mradi wa Mgango – Kiabakari wa shilingi bilioni 70 mradi ule unaenda kuhudumia wananchi 150,000 na kuendelea, lakini pia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutupa mradi mwingine wa maji, ukienda pale Bunda tumepata mradi wa maji wa shilingi bilioni 10 ule mradi wa chujio la maji utaenda kuhudumia wananchi takribani 160,000 na hapa nimpongeze sana dada yetu Ndugu Ester amekuwa ni Mkurugenzi mzuri ambaye anasimamia vizuri miradi ya maji tunampongeza sana yeye pamoja na watendaji wa Bunda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumeendelea kupata miradi yam aji ile ambayo inaendelea kutekelezeka, tumepata miradi ya maji, maji vijijini miradi 38 na miradi hiyo tumepewa shilingi bilioni 24 na tayari shilingi bilioni 10 imeshakuja. Hiyo ni kazi kubwa na nzuri ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan chini ya Waziri makini, Mheshimiwa Jumaa Aweso unayepambana kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumeendelea kupata miradi ambayo inaendelea mpaka sasa kutekelezeka tumepata mradi wa miji 28 mradi ambao utaenda kuifanya Tarime Mjini, Tarime Vijijini lakini mpaka na Rorya wanawake wa Mkoa wa Mara kupitia mradi huo watapata maji, wanawake wa Tarime watapata maji, mama zangu wa Tarime Vijijini watapata maji. shilingi bilioni 134 Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka pale. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo hivyo hakuwasahau wananchi wa Serengeti kwa kuleta shilingi bilioni 20 kwa ajili ya mirafi ya maji wanawake, wakina mama, mama zangu wa Wilaya ya Serengeti wataenda kupata maji. Hii ni dhahiri kwamba Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kwa dhati kabisa kumtua mwanamke wa Mkoa wa Mara ndoo na hii ni utekelezaji mzuri wa Meneja wetu wa Mkoa wa Mara Meneja wa RUWASA kaka yangu ninakupongeza sana kwa namna ambavyo umepambana kuhakikisha unaisimamia miradi ya maji katika Mkoa wa Mara, wanawake wa Mara watapata maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwenu, ombi langu na ushauri wangu kwa Serikali ni kuhakikisha miradi ya maji inataklezeka kwa kuleta feda nyingi ili miradi ile iweze kukamilika tumsitie doa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyojitolea kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Mara wanapata maji, wananchi wa Tarime, wananchi wa Serengeti, wananchi wa Rorya, wananchi wa Butiama, wananchi wa Tarime Mjini, wananchi wa Tarime Vijijini, wananchi wa Bunda wanaendelea kupata maji katika kumtua ndoo mwanamama wa Mara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo ninaunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)