Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi nichangie Wizara hii ya Maji, lakini kwanza kabisa naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu aliyetujalia uhai leo hii tuko hapa na kuweza kuchangia katika Wizara hii.

Pili, nimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kweli Mama yetu tunadiriki kusema anaupiga mwingi japo watu wakisikia kwamba tunasema anaupiga mwingi wanakasirika, lakini ukweli ni kwamba Mama anaupiga mwingi lakini hasa katika adhima yake ya kumtua ndoo mama kichwani na hii imedhihirika katika Jimbo langu la Tunduru Kaskazini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Maji ndugu yangu, kaka yangu Mheshimiwa Jumaa Aweso kwa kweli anafanya kazi kubwa sana, sana, sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimshukuru Naibu Waziri wake kwa sababu anamsaidia kazi vizuri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na watendaji wote wa Wizara ya Maji hakika wanaitendea haki Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nianze kwa kuzungumzia maji Tunduru Mjini, maji Tunduru Mjini na Vijijini kwa ujumla wake kwa muda mfupi huu mimi nilipoingia madarakani jumla ya shilingi bilioni 12.321 na zaidi zimetekeleza miradi ya maji ya Tunduru Mjini pamoja na Tunduru Vijijini ambapo shilingi bilioni 7.4 na zaidi imekwenda kutekeleza maji Tunduru Vijijini kwa maana ya RUWASA, lakini shilingi bilioni 4.8 imekwenda kutekeleza maji mjini kwa maana ya TUWASA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimshukuru sana, sana, Mheshimiwa Waziri wa Maji Tunduru Mjini tulikuwa tunachangamoto kubwa sana ya maji na kulikuwa kuna lawama nyingi za watumiaji wa maji wengine walikuwa wanapelekewa bili na wansema kwamba tumeletewa bili, lakini kwa mwezi mzima hatujaona maji lakini tumeletewa bili na maji yanaweza kutoka mara moja, mara mbili kwa mwezi ama mara tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo changamoto ilikuwa ni kubwa sana, lakini baada ya ujio wa Waziri wa Maji ndugu yangu Mheshimiwa Jumaa Aweso alipoikuta changamoto ile pale pale alichukua hatua tena ilikuwa mbele ya Madiwani pamoja na DC wetu mchapakazi mkubwa katika Wilaya yetu ile ya Tunduru Mjini. Pale pale alichukua hatua kwa kutoa pesa za dharura jumla ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya kwenda kuboresha miundombinu ya maji pale mjini, lakini alitoa gari kwa ajili ya kuisaidia idara ile, lakini pia alitoa pikipiki 10 mpya kwa ajili ya kuwawezesha wale wataalamu wa maji ili kwenda kutatua matatizo kwa haraka zaidi badala ya kwenda kwa mguu. (Makofi)

Mheshimiwa Aweso tunakushukuru sana, sana, sana, lakini kama haitoshi pale mjini sasa hivi tunao mradi ambao tumesaini juzi tu leo ni siku ya tatu mradi wa shilingi bilioni 3.2 ambapo engineer yule, Engineer Kiwia amekwenda amefanya utafiti na amegundua eneo lenye mwinuko mkubwa zaidi ambapo mradi ule ukienda ukikamilika utakwenda kutatua changamoto ya maji katika kata zote saba za tarafa ya Tunduru Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaanisha kwamba mradi ule ukikamilika Kata ya Sisi Kwa Sisi itakwenda kunufaika na mradi ule Kata ya Nanjoka itakwenda kunufaika na mradi ule, Kata ya Majengo itakwenda kunufaika na mradi ule, Kata ya Nakapanya itakwenda kunufaika na mradi ule, Kata ya Mlingoti Mashariki itakwenda kunufaika na mradi ule Kata ya Mlingoti Magharibi itakwenda kunufaika na mradi ule.

Mheshimiwa Waziri lakini pia mimi nikuombe sana tena sana katika mameneja wa maji wote mjini waliowahi kupita Tunduru Mjini kwa kweli Engineer Kiwia anafanya kazi kubwa sana, tena sana nikuombe usituhamishie meneja huyu ndugu yangu Engineer Kiwia tafadhali sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitoka kwenye maji mjini naenda maji vijijini kwa maana ya RUWASA, kwa kweli hapa mama ameupiga mwingi mno, mno, mno. Maji vijijini kwa maana Kata ya Namwinyu tuna mradi ambao mpaka sasa umefikia hatua ya 70%; tunao mradi kule kwenye Kata ya Namwinyu tuna mradi wa shilingi milioni 450 ambapo utekelezaji wake upo katika 70%, lakini Kata ya Kijiji cha Ulia tuna mradi wa jumla ya shilingi bilioni 1.26 ambapo wenyewe tayari umekwisha kamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, kesho kutwa tu nikienda kwenye mwenge tunakwenda kuuzindua rasmi mradi ule na akina mama wanakwenda kuteke maji na hatimaye tutaimba nyimbo ya Samia, Samia, Samia. (Makofi)