Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Magu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa nataka nimpongeze Mheshimiwa Rais na kumshukuru sana kwa namna ya pekee ambavyo mmendelea kutupa miradi mingi ya maji ambayo kwa kweli nikuombe Mheshimiwa Waziri uandae utaratibu ili Mheshimiwa Rais aje afungue Mradi wa Maji Magu ambao umenufaisha wananchi 99%, lakini nikupongeze Mheshimiwa Waziri kwa kweli hatuna namna ya kukuelezea, lakini utasimuliwa kwenye historia ya nchi hii kwamba alikuwepo Waziri wa Maji Mheshimiwa Aweso na Makatibu Wakuu na Naibu wake Waziri pamoja na wakuu wa taasisi ambao wanakusaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nipongeze RUWASA, nipongeze pamoja na wataalamu wote watendaji ngazi ya mkoa pamoja meneja wangu wa Wilaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunao Mradi wa Bujora ambao tenki kubwa limekamilika na hapa ndipo naendelea kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa sababu tumepata shilingi bilioni tatu lile tenki lina cubic litre milioni tano na wameanza kutandaza mabomba kwenda sawa kwenye chanzo cha maji. Huu utakuwa ni mwarobaini kwa Mji wa Kisesa na Bujora ambao utanufaisha vijiji vya Kanyama, Bujora yenyewe, Wita, Igekemaja, Kitumba, Langi pamoja na pale Busekwa. (Makofi)
Kwa hiyo, niombe sana kwamba sasa baada ya kukamilisha kupeleka bomba kwenye chanzo sasa mabomba ya kwenda kwa wananchi ambao hawana mradi wa uliopo sasa nayo yaendelee kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Kata ya Bujora pamoja na Kata ya Kisesa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunao mradi wa Lutale - Langi ambao mwaka jana tuliuweka kwenye bajeti ya mwaka huu tunao malizia taarifa nilizonazo kutoka kwa Mkurugenzi wa RUWASA ni kwamba huu mradi utatangazwa mwisho mwezi wa sita. Kwa hiyo, niombe sana ni maradi ambao utanufaisha vijiji tisa tutamaliza matatizo ya wananchi kutoka Langi, Kageye, Itandula, Shilingwa, Sese, Ihushi, Matale, Igekemaja na vijiji vingine ambavyo vinazunguka karibu pale. Niombe pia mradi wa awamu ya pili Mradi wa Sola – Bubinza ambao kwa kweli ni mradi tumeanza kujenga chanzo kule Busega ambako kuna chanzo kizuri tayari na tunategemea sasa lijengwe tenki kubwa pale Sola la cubic litre milioni mbili na ule mradi utanufaisha hata Tarafa nzima ya Ndagalu baada ya ukamilika napo nimetaarifiwa kutoka kwa Mkurugenzi wa RUWASA kwamba utatangazwa mwezi wa sita mwaka huu bajeti unayomalizia na kwenye bajeti hii umo umewekewa fedha kwa hiyo nikiombe sana taratibu hizi zote ziweze kukamilika nao utanufaisha vijiji 21 na mradi huu utakuwa ni mradi mkubwa sana ambao utasaidia wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe miradi ambayo inaendelea Mradi wa Iseni – Nyang’anga – Buhumbi; Mradi wa Misungwi – Kitongo; Mradi wa Sagani - Mwamabanza pamoja na Mradi wa Lugee -Kigambana, miradi hii ipo asilimia kubwa. Mradi wa Lugee - Kigangama ambao utanufaisha Kata ya Nyanguge na Mwamanga, mkandarasi amekwisha kufanya kazi zaidi ya shilingi bilioni tano, amelipwa shilingi bilioni moja, bado shilingi bilioni nne na amejenga tenki, amesambaza mabomba, bado kujenga chanzo, nimemwona hapa Naibu Waziri wa Fedha, niombe Wizara ya Fedha ipeleke fedha Wizara ya Maji ili iweze kulipa wakandarasi na wakandarasi waweze kuendelea ili watu waweze kupata maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Iseni - Nyang’anga nao uko asilimia 90, unategemewa kupewa tu fedha za kumalizia ili wananchi waweze kupata fedha na namna pekee ya kuweza kumtua mama ndoo kichwani ni hii, lakini Wizara hii kwa kweli imetoa fedha kwa ajili ya kuchimba visima, visima hivyo vimechimbwa kwenye vijiji mbalimbali, tumeyapandisha maji kwenye matenki, tumeanza kusambaza kwenye vijiji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niombe Wizara hii kadiri ambavyo itaendelea kupata fedha tuweze kunufaisha wananchi kama ambavyo Wabunge wengi wameeleza kwamba sasa ni vijiji vichache ambavyo vimebaki havijafikiwa na maji. Tunaamini kwamba Serikali ya Awamu ya Sita ambayo imejipambanua kuhakikisha kwamba inawapatia wananchi maji tuone sasa kwenye hii bajeti, Mheshimiwa Aweso unapeleka fedha ili kuhakikisha kwamba fedha hizi zinanufaisha wananchi. (Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Boniventury.
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, niunge mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)