Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi, lakini pia nimshukuru Rais wetu Mama yetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya katika nchi yetu, lakini tatu nimshukuru Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na viongozi wote wanaoshughulika na sekta ya maji hasa viongozi wangu wa DAWASA pale Dar es Salaam. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ya Maji kupitia DAWASA katika Mkoa wa Dar es Salaam imefanya mambo makubwa sana. Kwanza nichukue nafasi hii kushukuru kwa miradi mikubwa ya upanuzi wa mtandao wa maji pale Dar es Salaam hasa katika Jimbo la Mbagala, zaidi ya shilingi milioni 389 zimetumika katika kuhakikisha miundombinu ya maji inawafikia wananchi na wananchi zaidi ya 200,000 wamenufaika na miradi ya maji katika maeneo ya Kimbangulile, Kizinga, Kijichi Mchikichini, Charambe, Makuka, Bamia, Msufini, Rufu, Moringe, Mji Mpya, Machinjioni A, Kokoto, Goroka, Kiponza, Rangi Tatu, Bugudadi na maeneo ya Nyambwela.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeyataja maeneo haya kwa sababu ni watu ambao muda mrefu walikuwa hawapati huduma nzuri ya maji, lakini sasa hivi kwa kupanuliwa mtandao wa maji wameanza kupata maji na kwa kweli na wao wanaishukuru sana Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, niishukuru sana Serikali kwa miradi mikubwa miwili ambayo inaendelea, mradi ule wa kutoa maji Mto Rufiji. Mradi ule utakapokamilika, naamini katika Jimbo langu la Mbagala matatizo ya maji yatakuwa ni historia lakini kuna ule mradi wa Bwawa la Kidunda ambalo ninamini linaenda kuongeza nguvu katika upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niendelee kuwapongeza na kushukuru huduma ya usafi na mazingira, katika Jimbo langu la Mbagala tumepata vyoo vya umma vinne ambavyo vimejengwa katika maeneo ya soko la Rangi Tatu, Mbande, Kampochea na maeneo ya Toangoma. Kwa kweli, Wizara pamoja na DAWASA kwa ujumla wamefanya kazi kubwa sana katika Jimbo langu la Mbagala lakini bado tunayo changamoto. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe sana Mheshimiwa Waziri, alitembelea pale Charambe, ameona lipo eneo halina mtandao kabisa wa maji ya DAWASA. Tunayo maeneo ambayo yana matatizo, maeneo ya Maji Matitu, maeneo ya Chasimba, maeneo ya Kilungule, maeneo ya Machinjioni B na Machinjioni C, maeneo ya Dovya, maeneo ya Kisewe na baadhi ya maeneo ambayo kwa kweli bado yamekuwa na changamoto ya maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukuombe sana ili Dar es Salaam ikamilike, wakazi wengi wa Dar es Salaam wanapatikana katika maeneo haya. Tukuombe sana katika hiki kipindi kilichobaki yapo mambo tunaweza tukayafanya maeneo haya yakapata maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja; tunacho kisima pale panapoitwa Mabomba Nane, eneo lile kile kisima kina maji mengi, maji yale tukiyaongezea booster pump yanaweza yakapeleka Kilungule, Chasimba na maeneo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo haya yamekuwa na matatizo ya maji, si kana kwamba hakuna visima, lakini maji yanayopatikana ni ya chumvi, hayafai katika matumizi ya binadamu. Pia eneo la Dovya ipo chemchem kubwa ya maji imeonekana pale. Tuwaombe sana, sisi Dar es Salaam tunafahamu hatujapata magari ya kuchimbia visima vya maji, lakini tuombe yatafutwe mazingira yoyote maeneo haya yaende yakachimbwe visima vya maji, kwa sababu vyanzo vya maji vimeonekana na bahati nzuri DAWASA wamepima wameona maji yale yanafaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, DAWASA wana water bowser, naomba water bowser zile zitumike vizuri ku-supply maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. (Makofi)