Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima kubwa kwa niaba ya wananchi wa Iringa Mjini, tunaomba tutoe shukrani zetu za dhati kwa huduma bora kabisa ya maji katika mji wetu wa Iringa. Upatikanaji wa maji Iringa Mjini ni karibu 98%. Huduma ya kutatua changamoto na matatizo ya wananchi yanafanyika kwa ustadi, utu na upendo mkubwa na kwa njia za kisasa kabisa za kidijitali. Mheshimiwa Waziri naomba sasa kwa ajili ya Iringa Mjini, kama unavyojua maeneo mengi ya mjini huduma za jamii kama shule na vituo vya afya, zahanati na hospitali zinatumika na watu wengi hata wa kutoka maeneo mengine ya majimbo ya vijijini. Shule zetu nyingi za kata ni za hosteli na ni kwa watoto wa kike. Maji ya bomba ni changamoto. Ninaomba muone kwa ngazi ya Wizara msaidie hizi baadhi ya shule za mjini zichimbiwe visima hasa zenye uwezekano wa kupata maji. Pili eneo la Ugele na Mosi tuchimbiwe visima virefu. Ahsante na nashukuru.