Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kuungana na Watanzania wenzangu wote kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia baraka zake kwa Taifa letu nyanja mbalimbali za ustawi wa kijamii kisiasa, kiuchumi, kidplomasia, amani na mshikamano, ahsante sana muumba wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kuungana na wananchi wa jimbo langu la Mbulu Mjini kushukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali yake nzima ya Awamu ya Sita kwa jinsi alivyotekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2020/2025 Mwenyezi Mungu awabariki sana, sisi wananchi wa Jimbo la Mbulu Mjini tutamlipa fadhila zake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2025 kwa kumpigia kura nyingi za imani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Jumaa Aweso - Waziri wa Wizara hii muhimu sana, nampongeza sana Mheshimiwa Andrew Kundo - Naibu Waziri, Katibu Mkuu Engineer Mwajuma Waziri, Naibu Katibu Mkuu na watendaji wakuu wa Wizara hii kwa ujumla wao na naipongeza pia hotuba nzuri sana ya Mheshimiwa Waziri aliyoiwasilisha mbele ya Bunge letu hivi punde.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kuipongeza sana Kamati yetu ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kwa taarifa yao waliyoiwasilisha mbele ya Bunge letu kwa kweli imefafanua hali halisi na changamoto mbalimbali na mapendekezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kutoa mchango wangu kupitia mapendekezo hayo bajeti ya Wizara hii muhimu sana; kwa kuwa tumefanikiwa sana kuchimba visima vingi sana kupitia RUWASA katika majimbo mbalimbali nchini hali iliyowapa matumaini makubwa wananchi wetu kupata huduma bora ya maji safi na salama maeneo mengi. Hivyo basi tunaiomba Serikali yetu ijitahidi kupeleka fedha zinazoombwa kwenye bajeti ya Wizara hii muhimu sana kwa 100%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi wa jimbo langu la Mbulu Mjini naishukuru sana Serikali yetu kwa kubuni mradi mkubwa wa maji wa Mto Tsoray katika tarafa nzima ya Nambis ambao utasaidia kutatuta tatizo la maji katika vijiji zaidi 28 katika Halmashauri ya Mbulu Mjini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ninaiomba sana Wizara kuharakisha utekelezaji wa mradi huu kwa kuwa wananchi wangu wanausubiri kwa haiba kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaishukuru sana Serikali kwa mpango wake wa kuchimba visima 900 nchini ambapo kila jimbo limefanikiwa kupata visima vitano. Hivyo basi tunaiomba Serikali yetu itafute fedha za kujenga miundombinu ya kusambaza maji kwenda kwa wananchi wengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja 100% na naomba kuwasilisha.