Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nimpongeze Rais mpendwa Mama yetu kipenzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuletea miradi mingi katika Jimbo la Lushoto ikiwemo miradi ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Lushoto lipo milimani na kwa bahati nzuri Mungu ametujaalia vyanzo vingi vya maji. Tunachohitaji kwa sasa ni miundombinu ya maji kama vile matenki pamoja na mabomba kwa ajili ya kusafirisha maji hayo ya mserereko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna chanzo chetu cha maji ambacho kina uwezo wa kusambaza maji kwenye jimbo lote la Lushoto isipokuwa kata mbili tu ambazo ni Kata ya Kilole na Ngwelo kati ya kata 15 za Jimbo la Lushoto na mradi huu ukitekelezeka na ukakamilika una uwezo wa kupeleka maji katika Wilaya ya Korogwe na Handeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ulishatembelewa na Mkurugenzi wa RUWASA na alishuhudia kuwa chanzo kile ni cha uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaomba mradi huu utengewe fedha kwenye bajeti hii ili wananchi wa Lushoto waondokane kabisa na kero ya maji na kwa bahati nzuri mradi huu umeshatengewa pesa za upembuzi yakinifu, ila sijajua mpaka sasa upembuzi huu uliishia wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja, pamoja na kuendelea kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Maji Ndugu Jumaa Aweso pamoja na timu yake yote kwa kazi kubwa wanayoifanya.