Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza na kumshukuru mpendwa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa fedha nyingi alizoidhinisha ziwekezwe kwenye miradi ya maji Vunjo takribani shilingi bilioni 12 ndani ya miaka minne. Ninapongeza pia Waziri wa Maji, Naibu wake, Katibu Mkuu pamoja na timu yake Naima Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa RUWASA na Mamlaka za Maji Mkoani Kilimanjaro kwa kusimamia vyema matumizi ya fedha hizi na miradi yenye thamani ikapatikana na hivyo kumtua mama ndoo kichwani kwa kiwango kikubwa kwenye Jimbo la Vunjo. Hata hivyo ninamuomba Mheshimiwa Waziri atoe fedha ili miradi inayoendelea kutekelezwa kwenye Kata za Mwika Kusini, Mwika Kaskazini, Marangu Magharibi na Marangu Mashariki ikamilishwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashauri utaratibu wa sasa wa kukatisha huduma ya maji mashuleni na kwenye vituo vya afya mara tu wanapochelewesha kulipia huduma hii iangaliwe upya.