Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipatia fursa hii nami niweze kuongea mawili, matatu, lakini kikubwa sana Waheshimiwa Wabunge wameongea, Bunge limeongea maana yake Watanzania wameongea na kikubwa zaidi wamepongeza kazi kubwa sana ambayo imefanyika.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo nasimama hapa nikiwa katika bajeti ya tano nikiwa Naibu Waziri, imani hiyo namshukuru sana kwa kunipatia na hiyo ni heshima kwa wananchi wa Jimbo la Bariadi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru sana kaka yangu Jumaa Hamidu Aweso. Kaka yangu huyu…