Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote kwanza nikushukuru wewe binafsi, lakini niwashukuru Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa michango yenu na ushauri wenu ambao na pongezi zenu ambazo mmezitoa katika Wizara yetu ya Maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuna maneno matamu sana ya kusema zaidi ya kusema ahsanteni sana na Mwenyezi Mungu awabariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kubwa ambalo ninataka kusema Waheshimiwa Wabunge mmechangia katika bajeti yetu ya Wizara ya Maji, niwaahidi kila Mbunge ambaye amechangia katika bajeti yetu ya Wizara ya Maji tutawajibu kwa maandishi ili kuhakikisha kwamba tunaleta kumbukumbu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kubwa nitumie nafasi hii nami niungane na Waheshimiwa Wabunge kwa dhati ya moyo kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hakuna hata mmoja ambaye asiyejua. Mimi nimepata bahati ya kuwa Mbunge katika kipindi cha miaka kumi sasa na mimi ni Mbunge hakuna sekta ambayo ilikuwa ya kero na lawama kama Wizara Maji. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri toa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii kusema dhati tu ya moyo, Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiyo suluhu ya matatizo ya Watanzania hasa katika kumtua mwana mama ndoo kichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya naomba kutoa hoja, ahsante sana. (Makofi)