Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Niseme kwamba mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria. Nashukuru kwa nafasi ya kuwa mchangaji wa mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama walivyosema wengine, tumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa aliyofanya kwa miaka hii katika sekta zote nchini. Ametujengea Waheshimiwa Wabunge heshima kubwa sana kwenye Majimbo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hakuna Jimbo unaweza ukazungumza habari ya miradi ya maendeleo kwa miaka minne ya Mheshimiwa Dkt. Samia, ametubeba sana. Kwa hiyo, kwa kweli kwa kuwa mtumishi namba moja wa nchi hii ameonesha standards nzuri, tunachotakiwa sisi wengine ni kuiga ili Watanzania wapate huduma hii ambayo Mheshimiwa Dkt. Samia anataka Watanzania wapate. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Simbachawene amepata sifa nyingi sana hapa. Mimi kama Mjumbe wa Kamati nina-confirm. Kama kuna Mheshimiwa Waziri ambaye tunashirikiana naye vizuri sana kwa level ya Kamati na kutoa ushirikiano wa mfano ni Mheshimiwa Simbachawene. He is very humble, hana dharau. Ukimwomba saa yoyote kukutana, mnakutana, na anakusikiliza vizuri sana. Kwa hiyo, kwa kweli mzee siyo bure umedumu kwenye Bunge hili. Nakuombea maisha marefu zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Naibu Waziri wake ni chuma. Ame-catch up haraka sana. Tangu ateuliwe kwa kweli Kamati imefurahia kazi zake, na tumezunguka naye kwenye miradi mingi ya maendeleo. Anafanya kazi nzuri sana na yupo kwenye mikono salama ya ulezi na atafika mbali brother. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru Katibu Mkuu na viongozi wote wa Wizara hii kwa ushirikiano waliotoa kila wakati kwa Kamati, na ushauri ambao tumetoa kama Kamati wamekuwa wanachukua kila wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utumishi duniani; watumishi ndio engine ya kuendesha Serikali. Kwa hiyo, watumishi ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa. Pale nchi yetu inapoongeza fursa na uchumi wetu unavyoongezeka, tukiendelea kujali maslahi yao na kuboresha mishahara yao na maslahi, tutatengeneza public services nzuri sana ambayo itatoa huduma nzuri sana kwa Watanzania na utawala bora utakuwa bora zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nao kwa sababu hali ya nchi yetu wanaifahamu, na wanajua, ikiongezeka tuwajali, kuanzia Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji, watu wamezungumza, na watumishi wote, na Walimu wamezungumza hapa ma-guru kabisa, na kazi za walimu kwa kweli ni kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, in fact, siku hizi hata walimu ukiacha kazi zile alizosema Mheshimiwa hapa, wanafanya kazi za ulezi. Siku hizi kazi yetu sisi ni kupeleka tu watoto shule. Tulikuwa tunalipa ada na Mheshimiwa Dkt. Samia ameondoa ada; sasa hata kazi ya wazazi siku hizi ni kuzaa tu halafu na kupeleka watoto wakafundishwe elimu; kusoma, na kuandika lakini pia na malezi siku hizi wanapata kwa walimu wetu. Kwa hiyo, walimu ni watu muhimu sana kwa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna Taifa limeendelea bila kuwa na walimu. Wote waliokaa hapa wamepitia mikono ya walimu na wametajwa watu wengi hapa; Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Spika Mwalimu wangu, na akina Mheshimiwa Dkt. Balozi Kakurwa, wapo hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa likitaka kujenga misingi imara, ni lazima tuwajali wale watumishi ambao ndio wanaotuwekea misingi kwenye Taifa. Kwa hiyo, kwa kweli kama walivyosema Kamati, Watumishi wa Umma ni engine kwa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, tunachotegemea na sisi ni kwamba watoe huduma nzuri kwa Watanzania. Watanzania wanataka huduma nzuri sana. Uwe daktari au mwalimu uwe na lugha nzuri tu. Mkianzia kwa viongozi wenu wao ni humble, Makatibu Wakuu, Mheshimiwa Waziri Mkuu hapa Mheshimiwa Dkt. Samia. Sasa kama hawa wakubwa ni humble kiasi hicho, wewe ambaye ni mtumishi uliyepata ajira, utaachaje kuwa humble na ukatoa huduma? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanya hivyo, na kwa sababu unajua ajira imekuwa jambo kubwa sana, na ni kwa sababu moja tu, nchi yetu tangu tumepata uhuru ongezeko la vijana wanaosoma limekuwa ni kubwa sana, kila mahali, hata kuliko capacity ya Serikali kuajiri. Kwa hiyo, kwenye suala hili la ajira, na kama walilivyoshauri Kamati, tufanye huu mjadala wa Kitaifa kila wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili siyo suala la utumishi pekee, nadhani tuwe na makongamano ya Kitaifa, tuwe tunazungumza habari ya ajira na namna bora ya kuweka sawasawa ili liwe jukumu letu wote. Tupate mawazo kutoka kwa Watanzania kuhusu namna ya kufanya ili suala la ajira lipate mawazo mengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana, kama walivyosema Kamati na Waheshimiwa Wabunge hapa, kwamba tukiwa na taasisi bora ambayo ndiyo inaratibu suala la ajira likaongeza uwazi, likaongeza professionalism na mambo mengi, itaondoa manung’uniko. Isipokuwa na uwazi mzuri sana, itaanza kujenga matabaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namna ya pekee ya kuondoa hilo ni kuwa na taasisi moja, kama walivyopendekeza Kamati na Waheshimiwa Wabunge hapa, ambayo ndiyo inajengewa misingi ya kutengeneza suala la ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ajira, ni utaifa. Tunataka tuone Taifa, tukiona ajira; tunataka kuona inclusivity, na tunataka kuona watu wanaojitolea. Kujitolea ni suala la kizalendo. Tunataka ajira hizi zi-reflect umoja wa Taifa letu. Tusipokuwa na chombo maalumu ambacho kina-vet hii process tutatengeneza matabaka ambayo hayana maana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama walivyosema Kamati, taasisi yetu inayohusika na mambo ya ajira ikipewa jukumu hili nao wakaongeza creativity kwenye ajira zetu, nadhani Watanzania watafurahi na kila mtu ataridhika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila Mheshimiwa Mbunge hapa leo umemsikia, kila mtu angetaka leo katika ajira zinazotoka aone angalau vijana wawili au watatu wanatoka kwenye Jimbo lake, Kwa misingi hiyo hiyo ya kuendeleza utaifa na inclusivity.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu TAKUKURU, wamekuwa creative sana. Ule mradi wao wa kusema TAKUKURU Rafiki, ukiendelezwa zaidi; unajua tunachotaka ni kwamba badala ya kuanza kukamatana na kusubiri mtu afanye kosa akamatwe, tujenge vijiji, na tuwe na wenyeviti wenye weledi wa kufanya kazi zao vizuri sana. Kwamba leo tuwe na role modal ya kijiji ambayo unaweza mkatupeleka tukasema huyu mwenyekiti amefanya kazi zake vizuri sana na wenyeviti wote wanatakiwa wafuate hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii TAKUKURU Rafiki sasa, ulikuwa ni ubunifu mzuri sana, na ninampongeza Mkurugenzi wa TAKUKURU na Taasisi yote ya TAKUKURU kwa kuja na mpango huu wa TAKUKURU Rafiki. Tunataka taasisi zetu ziwe bora zaidi, tunataka utawala bora uwe bora zaidi. Kwa hiyo, wakati mwingine tu-invest kwenye kuwafundisha zaidi na kujenga uwezo wao kama walivyosema wengine hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamesema watu kuhusu vyuo vikuu. Vyuo vikuu vinahitaji independence kabisa, nami ninakubaliana. Alishasema Mheshimiwa Prof. Kitila hapa; mimi si mnywaji wa wine; alisema hivi, wine inavyozidi kukaa zaidi ndivyo inavyozidi kuwa bora zaidi. Nami nakubaliana naye. Profesa anavyozidi kuwa aged ndivyo anavyokuwa bora zaidi. Kwa hiyo, kuna wakati mwingine badala ya kusema tu tuwaachie tutengeneze mpango ambao kuna maprofesa, tutakubaliana huyu aendelee hata akiwa na miaka 100, why not. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi nyingine duniani kuna Profesa anakuja na wheel chair kwenye lecture theatre huku akiwa na over 100 years, but it doesn’t matter. Hata hivyo, haiwezekani kwamba ni kwa every professor, no. Lazima tutakuja na mpango maalum wa kuwa-recognize wale gurus kwenye maeneo fulani fulani. Awe ni mwalimu bingwa, awe ni Profesa ama awe ni Jaji Mahakamani. Kwenye sekta zetu hizi tukiweza kulinda hiyo, tutakuwa tumeweka msingi wa Taifa na Taifa letu likawa bora zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapotengeneza ajira za nje huko, lazima kuwe na freedom ya universities ili tuweze kuleta maprofesa kutoka nje, ili tuweze kuandaa vijana waweze kuajirika huko duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, nakushukuru sana.