Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha mchango wangu kwa maandishi. Kwanza, natoa pongezi kwa Wizara ya Nishati kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa na umeme wa uhakika, kipekee katika Jimbo la Iringa Mjini ninaloliwakilisha.
Mheshimiwa Spika, pili, kwa kuwa suala la kusambaza umeme ni kutoa huduma chochezi ya ukuaji wa uchumi nchini na kwa kuzingatia kuwa mipaka ya ugawaji wa kiutawala wa nchi yetu huwa hauzingatii kipato cha wananchi wetu, basi ni muhimu TANESCO wakatengeneza formula yao ya usambazaji wa umeme ukilinganishwa na kipato cha kiuchumi halisi cha wananchi kwamba wale wananchi wanaoishi ndani ya miji, lakini wana kipato kidogo waunganishiwe umeme kwa bei ya vijijini zikiwemo peri urban areas. Mfano, maeneo ya Mitaa ya Ugele, Msisina, Mtalagala, Kigungawe, Mosi, Wahe, Ulonge ndani ya Jimbo la Iringa Mjini.
Mheshimiwa Spika, tatu, maeneo ya mijini yaliyoanishwa kama vitongoji 15 au mitaa 15 katika maeneo ya mijini na kutakiwa kupewa umeme yafikishiwe umeme au ule mpango wa peri urban utekelezwe. Mfano maeneo ya Mitaa ya Ugele, Msisina, Mtalagala, Kigungawe, Mosi, Wahe, Ulonge ndani ya Jimbo la Iringa Mjini.
Mheshimiwa Spika, nne, tunaomba TANESCO iongezewe fungu la usambazaji umeme kama ilivyo kasi ya kufikisha umeme, basi iende sambamba na usambazaji wake. Kwa kuwa, maendeleo nayo yanaibua changamoto nyingine, watu wanavyoona umeme umefika haujasambazwa inazua tena malalamiko.
Mheshimiwa Spika, tano, suala la mafuta tunaomba ukaguzi ufanyike kwa uhakika kwa kuwa baadhi ya vituo vya kuuzia mafuta vinauza mafuta machafu yanayowatia hasara wananchi kwa kuharibu vyombo vyao vya usafiri. Hii inadumaza ukuzaji wa uchumi kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja.