Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Bahati Khamis Kombo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. BAHATI KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kukupongeza wewe kwa kuliongoza vyema Bunge. Pia nampongeza Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake uliotukuka.

Mheshimiwa Spika, nielekee katika mchango wangu. Wapo wananchi mpaka leo bado umeme haujafika. Naomba Serikali ichukue juhudi za makusudi ili waweze kupata umeme. Serikali imejielekeza kuboresha nishati ya kupikia ili wananchi hasa akinamama waachane na kupikia kuni ili waendelee kutunza mazingira, Serikali kufanya utaratibu wa kuongeza majiko ya gesi kwa wale ambao hawajafikiwa waweze kufikiwa na tuwaombe wanaouza mitungi ya gesi, wapunguze bei ili waweze kununua.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.