Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya kuhakikisha sekta ya nishati inaendelea kufanya kazi kwa kuipatia fedha za kutosha. Pia nampongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko pamoja na Naibu Waziri wake Mheshimiwa Judith Kapinga pamoja na Watendaji wote wa Wizara hii kwa kazi nzuri ya kuwahudumia Watanzania.
Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kilimanjaro una mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa. Kupitia bajeti hii, tunaomba Serikali iweze kukamilisha usambazaji wa umeme katika vitongoji ambavyo bado havijaunganishiwa umeme. Hii itasaidia kuinua kipato na kuboresha maisha yao.
Mheshimiwa Spika, napendekeza mambo yafuatayo yazingatiwe katika bajeti:-
(a) Kuongeza uwekezaji wa umeme vijijini (REA) ili kuunganisha umeme kwenye yale maeneo ya Mwanga-Same na Rombo ambayo bado havijafikiwa na umeme na kuhakikisha upanuzi wa miundombinu ya umeme vijijini unatekelezwa kwa kasi.
(b) Kuhamasisha na kuwezesha matumizi ya nishati mbadala Mkoa wa Kilimanjaro una fursa kubwa ya kutumia nishati jadidifu kama jua na biogas. Bajeti itenge fedha za kusaidia wananchi hasa wakulima na wafanyabiashara wadogo kupata teknolojia hizo.
(c) Kugawa majiko ya gesi kwa kaya za kipato cha chini ili kulinda mazingira ya Mlima Kilimanjaro dhidi ya ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa. Serikali itenge bajeti mahsusi ya kugawa majiko na mitungi sambamba na elimu ya matumizi salama. Hatua hii itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira kuhifadhi vyanzo vya maji na kukuza utalii endelevu.