Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

Hon. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2024

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu Mwenye Enzi na Utukufu kwa kuniwezesha kusimama katika Bunge hili Tukufu kwa mwaka huu 2025. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupitishwa kwa kishindo na Wajumbe wa Mkutano Maalum wa CCM kuwa ni mgombea pekee wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami kama Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, nasema kwamba Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan hatukumpitisha kwa sababu tu ndiye Rais aliyepo madarakani, wala hatukumpitisha kwa sababu ni Rais mwanamke kwamba tuna hamu ya kuendelea kuongozwa naye, bali tumempitisha kwa kazi kubwa za kishindo za utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo mojawapo ambalo linanifurahisha katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ni katika vile vipaumbele alivyovitaja kwenye kutengeneza uchumi shindanishi, uchumi shirikishi na uchumi fungamanishi. Jambo hili limetekelezwa kwa kishindo na Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee, kupitia TARURA nimeona jambo hili la kuhakikisha wananchi wanashiriki katika kujiletea maendeleo yao, nalo limefanyiwa kazi kwa kupitia kile kilichoitwa Samia Bond au Infrastructure Bond. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI anisikilize kwa makini. Nina ushauri kidogo kuhusiana na jambo hili la Infrastructure Bond au Samia Bond kama ambavyo CRDB imeiita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposhauri tutumie Infrastructure Bond ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika uchumi wao wa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu hatukumaanisha fedha itoke kwa Commercial Bank. Jambo hili tulitamani lifanywe na TARURA yenyewe kwa kushirikiana na BoT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la hili jambo ni kuhakikisha tunapunguza madeni kwa wakandarasi ili kuwawezesha kuwa liquid kwa kupitia Benki Kuu na TARURA wenyewe, wakusanye hizi fedha za wananchi wenyewe wazipeleke kwenye BoT. Ile fedha irudi kwa TARURA kuweza kutengeneza barabara zetu na kuwalipa wakandarasi kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha hii inapotoka kupitia Commercial Bank, shilingi bilioni 150 ambayo inamfanya banker ampe mkandarasi, ile advance payment mara anapoonekana ame-win tender kule TARURA, tunamwongezea mzigo mkandarasi wa ndani kwa sababu Commercial Bank inamtoza riba kwa fedha ambayo inampa. Kama fedha hii wananchi wangeipeleka BoT kama bond nyingine ambazo zinawekwa BoT, then ikirudi kupitia TARURA inaweza kuwasaidia wakandarasi wazawa kuliko ambavyo imepelekwa kwenye Commercial Bank. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba sana suala hili la Infrastructure Bond lifanyiwe marekebisho, lisipitie Commercial Bank kwa sababu tunawaongezea mzigo wakandarasi wa ndani na wala haliendi kwa maana pana ya kutatua changamoto ya madeni mengi ambayo Serikali inayo kwa wakandarasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo lingine ni kwamba tunayo Fuel Levy ambapo Serikali inakusanya almost 1.5 trillion per year. Kwa hiyo, tunapochukua zile bond, wananchi wakiweka BoT, ile Fuel Levy inaweza ku-service ile bond kwa maana ya zile interest kila baada ya miezi sita ambayo mwananchi anapaswa kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Fuel Levy inakwenda kurudisha ile interest ya six months ambayo mwananchi anatakiwa akalipie, lakini siyo kuchukua shilingi bilioni 150 of which is very minimum amount of money kuiingiza kama Infrastructure Bond. Jambo hili hatulifanyi sawasawa na lengo linalotakiwa kuhakikisha wananchi washiriki kwa upana wake, katika uchumi fungamanishi na uchumi shirikishi. Haiwezekani kupitia utaratibu huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana TARURA, jambo hili wakalibadilishe. TARURA na BoT washirikiane kukusanya fedha kutoka kwa wananchi na zirudi kama Infrastructure Bond. Ninachoweza kusema ni nini? Tumeshuhudia na hapa Waziri wangu Mheshimiwa Lukuvi ni shahidi, wananchi kibao wanarudi na fedha zao BoT wakitangaza bond. Maana yake fedha za wananchi zipo ambazo zinaweza kuingia kwenye Infrastructure Bond, lakini utashangaa tunakwenda kuji-confine kwenye Commercial Bank kumrudishia mzigo mkandarasi wa ndani. This is not fair. Tunaomba tulirekebishe. Ilani ile ya Chama cha Mapinduzi ilikuwa na dhamira njema, tusilipeleke jambo hili kibiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba kushukuru, ahsante sana. (Makofi)