Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songwe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia fursa ya kuchangia Wizara hii. Huwa nasema miaka yote kwamba Wizara ya Elimu ni Wizara yangu. Naomba ku-declare interest kwamba mimi mwenyewe ni Mwalimu, na uhai wa maisha yangu yote kwa kweli yametokana na Wizara ya Elimu. Nimeishi kama Mwalimu na vilevile nimeshawahi kutumika kama Naibu Waziri wa Elimu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo nichangie tu kwamba cha kwanza naomba niipongeze sana Serikali kupitia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo tunaendesha elimu yetu nchini na namna ambavyo Serikali imewekeza sana kwenye Wizara hii ya Elimu. Hata huko TAMISEMI tumeona mambo yanavyokwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Elimu, kaka yangu Mheshimiwa Prof. Mkenda pale, na ndugu yetu Naibu Waziri pale kwa namna ambavyo sasa hivi wanaiendesha Wizara ya Elimu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nimekuwa mhanga mkubwa sana na matamko ya huko nyuma tulivyokuwa tukienda, lakini hii miaka miwili nimekuwa naona tumeacha kabisa matamko matamko ya Wizara ya Elimu, sasa hivi yamepungua. Kila tunapofikia Januari unaona kuko salama, tunapofikia Julai kwenye mihula, tuko salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sisi huko tunaokuwa tunaishi na watoto huko na tunaishi na walimu, nami ni kiongozi wa shule za private hapa nchini, na-declare kabisa kwamba sasa hivi kuna amani na ndiyo maana mnaona hata leo watu wa TAMONGSCO hapa hawapo, watu wa TAPIA hapa hawapo, ni kwa sababu huko kwetu tayari kuna amani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namshukuru sana Mheshimwia Profesa Mkenda pamoja na Katibu Mkuu, na Naibu Waziri, na viongozi wote ambao wapo pale Wizarani. Sasa hivi wanashirikisha na wanatusikiliza.
Mheshimiwa Naibu Spika, hiki kilikuwa ni kilio cha mara kwa mara toka mwaka 2010, tunalia hapa kwamba jamani hebu mwashike shule za private na sisi shule za Serikali tukae pamoja tuweke mtaala pamoja. Tunashangaa nchi inakwenda pamoja, kwa sasa tunawafundisha watoto wetu pamoja. Watoto wetu wote wanasoma huko, kwa hiyo, lazima twende pamoja. Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, zamani tulikuwa tukisimama hapa, tuko na akina Rweikiza hapa, na akina Marehemu Ester Mahawe, yaani tunakuwa tumekasirika kasirika hivi, Waziri alikuwa hatuangalii vizuri. Leo hii Mheshimiwa Waziri nampita tunasalimiana, tunaongea jambo linaeleweka; namshauri anasikia; Mheshimiwa Naibu Waziri tunakunywa naye chai pale tunashauriana, tunasikilizwa, mpaka nao wenyewe wanatushauri na sisi tunasikia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii tunapokwenda kwenye Sera Mpya ya Elimu, naona kabisa tuko pamoja. Mheshimiwa Waziri siku moja tulikaa wote pale kantini nikawa najaribu kumpa mawazo ya namna kwamba hizi shule za private kama ambavyo nimesema, sasa hivi shule nyingi zimekosa wanafunzi huko kwa sababu ya elimu bure.
Mheshimiwa Naibu Spika, elimu bure inakwenda huko na wazazi wana-opt huko na kwa sababu tuna walimu wazuri Serikalini, tuna vitabu vizuri, tuna mtaala mzuri naye anasimamia elimu vizuri. Kwa hiyo, wazazi wengi wana-opt kwenda huko. Vilevile, madarasa ambayo yamebaki empty kuna madawati yapo huku, kuna walimu vilevile wapo. Hebu warudi sasa wageuke nyuma waweze kurudi huku sasa waanze kujaza watoto kule kwa sababu ni jambo dogo tu kufanya calculation.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna-calculate kwamba hii shule ina madarasa labda 10, walimu kadhaa mnaweza aidha mkanunua au mka-share na yule mmiliki wa shule mkafanya ili mambo yaende, kuliko kila siku tunapeleka fedha kwa ajili ya kujenga tu kumbe kuna shule nyingine bado ziko tu ambazo zimekaa empty na mambo yanaweza yakaenda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wenzangu nimeona wamechangia hapa kuhusu hii Sera Mpya ya Elimu ya mwaka 2014 mpaka sasa. Nataka tu niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, tulipokuwa tunaanza mfumo wa MEMKWA, MMEM na MMES, mimi nakumbuka nilikuwa Mwalimu na nilikuwa headmaster wakati ule.
Mheshimiwa Naibu Spika, tulihangaika sana na namna ya kuanza, lakini leo hii tunaona matunda ya MEMKWA, tunaona matunda ya MMES tunaona matunda ya MMEM. Hata hii Sera Mpya tunapokwenda, baada ya miaka 10 ijayo tutakuja kuona mambo yatakavyokuja kuwa mazuri baadaye.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kama Serikali haiwezi kwamba siku moja hii tayari itakuwa imeweza kwenda kule Chunya ikaweka madarasa yote yana Amali, iende Bukoba ikaweke madarasa yote ya Amali, ije Dodoma kwa wakati mmoja, hapana. Ndiyo maana Serikali imetoa fedha, kila mkoa tumepata shule moja kwa jili ya amali.
Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani Wabunge wote hapa mnahakikisha kwamba kila mkoa Mheshimiwa Rais ametoa fedha ili kila mkoa uwe na shule moja kwa ajili ya elimu ufundi kwa ajili ya Amali. Kwa hiyo, tunakwenda huko na baadaye tutakwenda sasa kila wilaya ipate hiyo shule na baadaye kila kata kama ambavyo tumekwenda kwenye MMES na MMEM.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tuwe wavumilivu, mambo haya yanaenda pole pole na ndiyo maana nilikuwa nimesema kwamba hata kwenye shule za private tupeni uhuru twende benki. Mkituhakikishia nyie kwamba sisi twende benki tukakope vifaa, tukakope mashine, watu wa carpentry, watu wa nini, twendeni huko tukakope mafundi umeme na tujenge vifaa vile.
Mheshimiwa Naibu Spika, tukishaweka kwenye shule, je mtatuletea watoto ili watoto wale waweze kusoma haraka kuliko tunavyoweza kuchelewachelewa hivyo wakati tuna uwezo sisi wa kufanya vitu kama vile? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kwenye shule yangu Mheshimiwa Waziri alishawahi kunishauri kwamba, “njoo Wizarani tukupe barua uende ukakope hela benki, ukienda CRDB wanakupa hela shilingi bilioni moja, unaenda kununua vifaa kwa ajili ya watoto wako wa chekechea wale, nursery mpaka huko primary ili waweze kuanza kufundisha elimu ya Amali.” Hata hivyo, sasa hivi tunaogopa kwa sababu hawajaturuhusu bado na hata akiniletea watoto, atashangaa baadaye wamehama.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuhakikishiwe kwamba tukifanya hivyo tunaweza tukapata wanafunzi ili tuendelee kuwafundisha. Ni Watanzania wote kwa pamoja tusaidiane kama ambavyo sasa hivi wanatusikia, nasi tusikiwe kwamba tuanze kusaidiana. Sasa shule za private zipewe uhuru, tuletewe wanafunzi, sisi tuwafundishe kwa sababu sisi walimu tunao na mambo yataenda vizuri sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Mheshimiwa Waziri kuhusu masuala ya VETA yanafanana fanana na elimu ya ufundi hii. Kule Jimboni Songwe mimi nimepewa VETA mwaka huu sasa ni wa tatu tunajenga, lakini iko very slow. Tunaona yaani fedha haziji mpaka wameezeka tu, lakini haijaanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama Mheshimiwa Waziri angeweza kunisaidia, tupate fedha kidogo kwenye bajeti yake hii, angalau basi na sisi tuanze kwa sababu naona wilaya nyingine VETA zimeanza, lakini kule Songwe kwa kweli bado kunasuasua. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nimesimama hapa nimetoka kantini kule, kuja kumpongeza tu Mheshimiwa Waziri namna ambavyo ameituliza Wizara ya Elimu. Yaani sikuwa na chochote, ndiyo maana unaona naongea hapa kwa kumpongeza tu na Naibu wake. Kwa kweli Wizara imetulia.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nirudie tena, Wizara ya Elimu sasa imetulia na nchi nzima inisikilize na walimu wenzangu wa shule za private wanisikilize; Katibu Mkuu, Kamishna wa Elimu, mzee nani pale Wizara wameituliza, na hii yote ni kwa sababu walitusikiliza ushauri wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tulimwambia Mheshimiwa Waziri sasa hivi hakuna kutoa waraka wowote bila Waziri kuuona. Huyu ni mwanasiasa, anajua nchi ilivyo huko nje. Kamishna anapotoa waraka wowote; sijui watoto wasilale kwenye mabweni, mabasi sijui nini, yaani kulikuwa kama vile kuna vurugu vurugu hivi, kila mtu anajichukulia.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikaja nikamwambia, “Mheshimiwa Prof. Mkenda, wewe ndio Waziri wa Elimu. Tutakuwa tunakusema wewe kumbe wanaharibu watu wako wa chini.” Kwa hiyo, nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri ashike hiyo kamba na ninamwombea Mungu kule Rombo wamrudishe aendelee kuwa Waziri wa Elimu. Ahsante sana. (Makofi)