Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia fursa hii nami niweze kuchangia katika bajeti ya hii ya Wizara ya Elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa ambayo unaifanya, kwa kweli umejitahidi sana kuhakikisha tunakwenda na mafunzo ya amali na tunakuwa na wanafunzi ambao wanaweza kufanya kazi kwa mikono yao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa uthubutu mkubwa ambao ameufanya kwa kuhakikisha kwamba, tunakuwa na sera nzuri, lakini tunakuwa na mitaala ambayo itakuwa inalega ujuzi ambao wanafunzi wetu wataweza kuupata pale ambapo watafundishwa ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia napongeza, kwa kuwa na Vyuo vya VETA ambavyo vimeweza kuanzishwa na wanafunzi walio wengi watakwenda kule. Sasa, sambamba na kuwa na hivyo Vyuo vya VETA, ushauri wangu waende sambamba na kuandaa wakufunzi watakaokwenda kufundisha wanafunzi hao, ambao watakuwa wanaweza kufundisha kwa ubora kama ilivyokuwa hapo awali. Pia mweze kuendana na vitendea kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na changamoto kubwa sana za vyuo vingi kutokuwa na vitendeakazi vya kufundishia hayo mafunzo ya amali. Sasa, katika bajeti yake naomba aweke bajeti maalum kwa ajili ya vitendeakazi pamoja na karakana ambazo zitatumika kuweza kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi ambao watakuwa wanafundishwa katika vyuo hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii elimu ya amali inatakiwa kuwa elimu ambayo ni bora kabisa. Sasa, ombi langu wale wadhibiti ubora ambao wapo, kama mtaweza kuwawezesha ni kujumu la Serikali kuwawezesha wadhibiti ubora kwenda kufuatilia udhibiti ubora wa hiyo elimu inayotolewa, kwa sababu tutasema tuna hiyo elimu ya amali, lakini kama wadhibiti ubora hatutawawezesha ipasavyo, hatutawapatia fedha, tutakwenda kuwa na jambo lile lile, kwa sababu elimu ili iwe nzuri ni lazima kuwe na wadhibiti ubora wanaongalia quality yake kwamba hii elimu ni bora ama siyo bora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumekuwa na elimu ambayo ipo, lakini tukijipima na nchi nyingine ama na wengine tunaona kwamba bado hatujafikia na ndiyo maana Mheshimiwa Rais akaamua kwamba tutengeneze mitaala yenye mafunzo ya amali ambayo yatatufikisha hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninasisitiza wadhibiti ubora waweze kuongezeka. Kwanza mwaajiri wa kutosha, mwaandae wa kutosha na waweze kupewa tools ambazo zitakwenda kuwasaidia katika kuhakikisha wanakwenda hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niende katika kipengele cha changamoto ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika bajeti zetu. Mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024 Wizara ilikopa shilingi bilioni tano kwa ajili ya miradi minne ambayo ilikopea SEQUIP, GPE-Lens na EASTRIP ambayo ilitakiwa ifanyike, lakini kwa sababu tuliondoa hizo fedha hatukwenda kufanyia katika kazi hiyo, mwaka 2023/2024 tuliomba tena fedha tutakosa shilingi bilioni 124 na point. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tumekosa hizi fedha kwa sababu tulikopa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo, hatukuitekeleza ipasavyo, sasa tukaja tukaomba fedha tena tukanyimwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sikatai kuomba fedha na sikatai, lakini CAG ametuambia kwamba, wamebaini fedha hizo zilikwenda kutumika huko ambapo hawakuombea. Sasa kama siku nyingine tunataka kutumia hizo fedha, ni bora tukatumia fedha za ndani, lakini tusitumie hizo fedha kwa sababu zinakwenda kusababisha kukosa fedha hizo ambazo tulikuwa tunatakiwa tuzifanyie katika miradi ambayo tulikuwa tunaitaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naiomba Serikali iweze kuwa makini katika kuangalia namna hiyo, ili tuweze kupata fedha ambazo zinaweza kutusaidia. Kwa sababu sisi wenyewe hatuna bajeti ambayo inajitosheleza peke yake, tunategemea bajeti ya ndani na nje. Kwa hiyo, tunapoomba bajeti kwa kitu ambacho umekiombea, basi tupeleke malengo yetu kule tulikoombea. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti hii, tuna makubaliano ya bajeti za elimu katika ukanda wetu. Bajeti za elimu ziweze kufikia angalau 15% ya bajeti nzima ya Serikali. Kwa hiyo, tuna matarajio kwamba, Bajeti ya Serikali yetu nzima inaweza ikafikia shilingi trilioni 55. Sasa, bajeti iliyopita angalau tulipata shilingi 12.5%, lakini nimeona Mheshimiwa Waziri ameomba shilingi trilioni tatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikaangalia katika ile 15% tutafikia asilimia ngapi? Utaona kwamba hata nusu tunaweza tusifikie ambayo inatakiwa. Kwa hiyo, tunamwomba Mheshimiwa Waziri aangalie hivyo tunavyokubaliana kikanda, basi bajeti zetu ziwe angalau zinafikia hapo ili tuweze kwenda sambamba, kwa sababu hapa umeeleza kwamba, kuna elimu jumuishi ambayo inatakiwa iwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo elimu jumuishi ina mambo ya akili mnemba, masuala ya watu wenye ulemavu na masaula mbalimbali ambayo yapo kwenye elimu jumuishi. Sasa, hayo yote yatahitaji fedha, kama haitatosha ina maana tutaweka kwenye bajeti, lakini utekelezaji utakwenda kuwa siyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba tunapoangalia hizi bajeti na tunapoenda kwenye bajeti kuu, basi angalau isogee, ivuke, ifikie, hata kama haifiki, basi isiwe chini sana ya makubaliano ya kikanda ambayo tunakubaliana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la tatu ni vitabu. Nawapongeza wameweza kuandaa, Taasisi ya Elimu imeandaa vitabu vya kutosha, lakini kumekuwa na changamoto. Hivyo vitabu havifiki kwa wakati, na huu ni mtaala mpya. Sasa kama ni mtaala ulioboreshwa au mpya, walimu wanakuwa bado hawajaweza ku-capture mambo yanayotakiwa, hawajafundishwa wote. Kwa hiyo, vitabu vinapochelewa haviendi sambamba na mtaala unavyotakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba Serikali ipeleke mapema vitabu, mwaka unavyoanza na vitabu viwepo. Kama Taasisi ya Elimu inakosa fedha, basi iwezeshwe kusafirisha vitabu viweze kwenda kwa wakati, wanafunzi wale waweze kupata vitabu waweze kuvitumia ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)