Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba kujengwe shule za watoto wa kiume kama zile za watoto wa kike shule za mikoa za wasichana au katika shule zile zile za watoto wa kike ziongezwe na miundombinu kama ya mabweni kwa ajili ya watoto wa kiume. Hii ni kutokana na changamoto zilizopo za ukatili sasa zinakua kwa kasi hadi kwa watoto wa kiume.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia ili kutoa elimu katika usawa, basi usawa huo upimwe hata kwa watoto kupata fursa sawa za mazingira yanayotolewa elimu, ikiwemo kupata miundombinu ya mabweni kwa wote.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na umuhimu wa suala la afya ya akili, basi ni muhimu kuanzisha klabu za afya ya akili ili kuwasaidia watoto kujitambua, kuzalisha kwa tija, kupambana na changamoto na kutoa mchango chanya kwenye jamii. Mambo hayo ni muhimu kwa kila ngazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba katika kusimamia ubora, basi Shule ya Msingi Nduli ihamishwe ndani ya uwanja wa ndege, na watoto wapate muda wa kupata mafunzo mengine ya dini.