Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Zulfa Mmaka Omar

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. ZULFA MMAKA OMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, awali nianze kumshukuru Mungu kwa neema ya uzima. Pili, nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anazozifanya katika Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze mchango wangu kwa suala la watoto wanaopata ujauzito wakiwa shuleni. Suala hili limepatiwa suluhisho la watoto hao kurudi shuleni baada kujifungua, ila nahisi kwamba elimu juu suala hili bado inahitajika kwenye jamii, kwa sababu inaonekana bado watoto wengi hawajarudi shuleni kwa hofu za wazazi jinsi gani jamii itawaangalia. Kwa hiyo, ombi langu suala hili litolewe elimu ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kujenga madarasa mengi vijijini. Hili linaenda kuondoa msongamano wa wanafunzi wengi darasa moja, ila naomba kwa upande wa matundu ya vyoo, bado ni changamoto kwa watoto wa kike na watu wenye mahitaji maalumu. Naiomba sana Serikali walitupie jicho jambo hili kwa roho ya kipekee.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naunga mkono hoja hii.