Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakuu wa Mikoa aina ya Makonda ndiyo wanafanya nchi iyumbe kiasi kwamba mitaani sasa hivi watu wanasema nchi ina Marais wawili, wanakurupukia mambo. Tumeujenga muziki wa Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka 25 mpaka leo unatoa ajira halafu mtu kwa kutaka sifa tu anasimama kwenye podium anavuruga kila kitu kwa muda wa dakika 20. Mheshimiwa Mwenyekiti, vitu kama hivi haviwezi kukubalika na ndiyo maana tunasisitiza umuhimu wa viongozi wote ambao ni presidential nominees wafanyiwe vetting na Bunge. Mtu kama Makonda angepita kwenye Bunge hili kufanyiwa vetting asingepita kwa sababu kwanza hana adabu alimpiga Mzee Warioba, wote tunakumbuka na picha ipo. Mtu aliyempiga Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya Mwalimu Nyerere, anamkunja, leo hii unampa kazi nyeti kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni makosa makubwa sana. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, anatuhumu watu, kama kutuhumu watu yeye Makonda anatuhumiwa kwamba ni mtoto na yeye tumwambie kwamba aende kwa Mganga Mkuu wa Serikali akapimwe marinda. Kwa sababu tufike mahali tuendeshe nchi kwa misingi. Waziri Mkuu upo, Waziri wa Mambo ya Ndani upo, Mawaziri mpo, Waziri wa Sheria upo, Serikali ipo, sasa hii nchi tunaipeleka vipi, tunaiyumbisha. (Makofi/Kicheko) Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, tuliheshimu Bunge ndugu zangu. Bunge liheshimike sana, hatutajenga viwanda kwa kumkamata Mheshimiwa Lissu na kumfunga kila siku na kupata dhamana. Hatutajenga viwanda kwa kumweka Mheshimiwa Lema detention hata kama atakaa kule ndani miaka kumi iko siku atatoka kwa sababu Mandela alikaa kwa miaka 27 na akatoka. Ndugu zangu, hii nchi ni yetu sote, tunaipenda, tunaomba sana tusikilizane, kama walivyosema waliotangulia kwamba sasa mambo ya CHADEMA, CCM yakae mbali tuwatolee macho na tuwakaripie watu kama Makonda, wanakuja hapa wanavurugavuruga nchi wakati nchi ilikuwa inakwenda vizuri. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.