Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017

Hon. Alex Raphael Gashaza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017

MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia taarifa za Kamati hizi mbili, Kamati ya UKIMWI na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nianze kwa kupongeza Kamati hizi kwa kazi nzuri walioifanya na niwapongeze waliotangulia kuchangia. Mengi wameyagusa, mimi nijielekeze tu kwanza kwenye suala la elimu.
Mheshimiwa Mwenekiti, kama wengine walivyotangulia kusema hakuna namna ambavyo Taifa lolote lile linaweza kuendelea kama bado halijaweza kuelimisha watu wake. Kwa kutambua kwamba kupitia elimu ndipo unapoweza kuwa na rasilimali watu iliyo bora na zaidi hasa katika kujenga msingi. Ukijaribu kuangalia rasilimali hii muhimu tunaanza kuipoteza kuanzia darasa la saba, tunakuja sekondari kwa maana kidato cha nne pale ambapo tunajikuta tumehamasisha, tumejenga shule nyingi za kata tukitegemea watoto wetu waweze kupate elimu hii na waweze kuendelea hadi vyuo vikuu lakini kwa matokeo kwanza ya mwaka huu ya kidato cha nne unaweza ukaona ni rasilimali kiasi gani ambayo itabaki nyuma huku vijijini ambayo ni nguvu kazi vijana kama hatukuweka mpango mahsusi kwa ajili ya kuona ni namna gani ambavyo rasilimali hii tunaweza tukaiboresha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niishukuru Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wamejaribu kuweka mpango wa kuanzisha vyuo vya VETA. Niombe mpango huu usiwe katika karatasi tu, uwe ni mpango unaotekelezeka, vinginevyo kama tutaendelea kupoteza rasilimali hii muhimu, kila mwaka vijana wetu wanamaliza kidato cha nne, zaidi ya 60%, 70% wanabaki vijijini, hawana ujuzi wowote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoteza rasilimali hii muhimu na hasa ukizingatia tunajipanga sasa Taifa hili liweze kuwa linajenga uchumi kuelekea kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda. Hakuna namna tunaweza kufaulu kama tusipoweza kuiandaa hii rasilimali muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na huduma zinazotolewa katika shule zetu, kuna kitu ambacho napenda Kamati wajaribu kuangalia. Sijui maeneo mengine lakini katika Jimbo langu la Ngara mara kadhaa kumekuwepo na tatizo la radi hususani katika maeneo ya shule. Mwaka jana tulipoteza wanafunzi watatu katika shule ya sekondari Kanazi kwa kupigwa na radi, lakini pia katika Kata ya Nyamagoma tulipoteza wananchi watatu kwenye familia moja ambao wako karibu na shule ya msingi na maeneo kadha wa kadha. Kwa hiyo, niombeā€¦
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga hoja za Kamati zote mbili.