Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Katiba na Sheria

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Katiba na Sheria

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga hoja mkono. Aidha, naomba kuchangia katika maeneo mawili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ucheleweshaji wa kesi hususan za jinai Mahakamani ni tatizo kubwa sana ambalo linahusisha Wizara nyingine kuu za Mambo ya Ndani. Makosa ya mauaji ni moja ya makosa ambayo watuhumiwa wake wanakaa muda mrefu mahabusu. Nashauri Serikali iangalie upya utaratibu wa High Court Session ili kesi hizo zisichukue muda mrefu kama inavyochukua wakati huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mahabusu pia ambao wanahukumiwa kifo utekelezaji wake haufanyiki vizuri. Suala hilo likaangaliwe mawakili wa Serikali maslahi yao yaangaliwe upya. Mishahara na marupurupu yao ni midogo sana ukilinganisha na kazi zinavyofanyika.