Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa hatua madhubuti anazozichukua kuhakikisha kuwa kasi yetu ya uchumi inaendelea kukua kwa kusimamia mapato na kuyaelekezea katika sekta za kiuchumi na uzalishaji. Ni hatua za kupongezwa sana. Aidha nampongeza sana Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wa Wizara na taasisi zake. Naomba maelezo ya kina kuhusu yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ujenzi wa flyovers Dar es Salaam. Hii ni hatua ya kupongezwa sana kwa kuwa ujenzi wa flyovers ni jambo ambalo Serikali za awamu zote imetamani ilifanye. Ni hatua ambayo itawezesha harakati za kiuchumi katika mikoa ya jirani na Der es Salaam. Hata hivyo, wananchi wangependa kufahamu juu ya ujenzi huu sasa na tafsiri yake kiuchumi ukilinganisha na maamuzi ya Serikali kuhamia Dodoma. Ukiangalia kwa sasa foleni ya Dar es Salaam imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwepo wa mabasi ya mwendo kasi. Aidha, uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza foleni pale Dar es Salaam. Swali linakuja, je, hizi flyovers zitaleta economic returns ukizingatia sababu za uwepo wa foleni pale Dar es Salaam zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa? Je, isingewezakana fedha za ujenzi wa flyovers zikatumika kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali hapa Dodoma? Naomba maelezo ya kina ili wananchi wapate kuelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, uuzwaji wa hisa za Vodacom. Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kutokana na zoezi la uuzwaji wa hisa za kampuni za simu kuanza kutekelezwa. Mheshimiwa Waziri amesimamia jambo hili tokea marekebisho ya kanuni zake ingawa limechukua muda mrefu. Hata hivyo, mauzo ya hisa za Vodacom bado hayajatangazwa sana kwa wananchi kupata uelewa wake. Vilevile kuna hisia kwamba hisa za Vodacom ziko over priced ukilinganisha na thamani halisi ya kampuni. Tunaomba Wizara ikishirikiana na TCRA na Wizara ya Fedha na Mipango, waliangalie jambo hili kwa umakini ili kuondoa hisia hizi zilizopo.

Mheshimiwa Spika, tatu, Shirika la Simu Tanzania (TTCL). Napongeza hatua kubwa ya mabadiliko katika Shirika la Simu Tanzania. Mabadiliko haya yanapelekea Watanzania kunufaika na kujivunia kuwa na shirika lao wenyewe la simu. Hata hivyo, tunaomba, baada ya hatua hii TTCL iwezeshwe kimtaji iweze kuweka miundombinu sahihi kwenye simu iweze kushindana katika soko la mawasiliano. Changamoto kubwa tunayopata sisi Watanzania ni kutokana na huduma zisizoridhisha za TTCL. Kwa upande wa ISP, TTCL bado hawako vizuri despite ya kutumia miundombinu ya umma (fibre optic).

Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Pemba. Ingawa kwa muda mrefu jambo hili limekuwa likizungumzwa bado hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa hadi leo. Uwanja wa Ndege wa Pemba ambao umewekwa katika program ya ujenzi kupitia EAC, Waziri hajazungumza lolote kwenye hotuba yake. Naomba atupatie maelezo kama Waziri mwenye dhamana hii ya mawasiliano na ujenzi kuhusu uwanja huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.