Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Salma Mohamed Mwassa

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. SALMA M. MWASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwa Wizara imefanya mengi mazuri, kuna mambo machache ningependa kuchangia kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa barabara kuwa chini ya kiwango. Kuna barabara ambazo zimetumia hela nyingi lakini zimejengwa chini ya kiwango, hivyo basi zimepelekea upotevu wa fedha za Serikali. Sasa basi nashauri Serikali kusimamia Mainjinia na Contractors kwa umakini ili matatizo kama haya yasitokee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchakavu wa majengo ya Serikali. Majengo mengi ya Serikali yamechakaa, kutokana na kutokarabatiwa muda mrefu. Hivyo basi, nashauri Serikali itenge fedha kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya Serikali kupitia wakala wa majengo TBA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchache wa majengo ya Serikali, majengo ya Serikali ni machache hivyo basi inasababisha watumishi wengi wa Serikali hata Mawaziri kukosa nyumba za kuishi. Hii inatokana na uuzwaji wa nyumba za Serikali kwa viongozi ambao sasa wengi wao wamestaafu, hivyo basi napenda kuishauri Serikali itenge fedha ili kujenga nyumba nyingi ili kuziba pengo la nyumba zilizouzwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukarabati hafifu wa barabara, ukarabati wa barabara haufanyiki mara kwa mara, hivyo basi inapelekea barabara nyingi kubomoka na kupelekea kupitika kwa shida au kutopitika kabisa, hivyo basi napendekeza hela kwa ajili ya ukarabati wa barabara zitengwe za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria ya manunuzi kuathiri ujenzi wa barabara kwa wakati, hivyo kupelekea ongezeko la gharama za miradi ya barabara, kama vile upembuzi yakinifu kuchukua muda mrefu kupelekea ongezeko la gharama za miradi ya ujenzi wa barabara. Nashauri Wizara isimamie upembuzi yakinifu ufanyike kwa wakati na bila kuathiri miradi ya ujenzi wa barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa barabara Kifuru mpaka Mbezi mwisho, Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam ni kilometa sita, lakini Mkandarasi amepewa fedha za kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami kilometa nne tu. Sasa basi kilometa mbili zitabaki kabla ya kufika Mbezi mwisho. Hivyo naishauri Serikali itenge fedha ili kumalizia kipande hicho cha barabara cha kilometa mbili mpaka Mbezi kutoka Kifuru, kuliko ilivyo sasa haileti sura nzuri ya barabara hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.