Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimwa Mwenyekiti, Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wake 2010-2015 ilisema ujenzi wa zahanati katika vijiji na kata ili kuokoa vifo vya akina mama. Sera ya afya ni ya Wizara ingawa mtekelezaji ni TAMISEMI, lakini wananchi wanaitazama Wizara ndiyo inaona haitekelezi ili kumuokoa mama na watoto katika vifo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majengo ya zahanati hizo yapo katika vijiji na kata lakini yapo magofu bila ya Serikali kuyamaliza. Je, Serikali hilo mmeliona maana tulitegemea mwaka 2015 -2020 yawe tayari yanafanyakazi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Saratani inashindwa kufanya kazi zake kwani kipimo cha upimaji wa saratani ya matiti kimeharibika toka mwaka 2008 na akina mama wanapata taabu, inabidi kwenda vituo vya nje kwa matibabu. Hivi sasa Tanzania imekumbwa na kansa mbalimbali; kuna saratani ya matiti, ya shingo ya kizazi kwa wanawake. Pia kuna saratani ya tezi dume kwa wanaume limekuwa tatizo kwa Watanzania.

Mheshimiwa Waziri ninaomba utoe elimu ya kinga badala ya tiba na pia elimu ya kutumia chakula gani ili kujinusuru na saratani, elimu ndiyo itamsaidia Mtanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara iendelee kuhamasisha kufanya mazoezi Watanzania kwani Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan anahimiza mazoezi kwa kila Mkoa katika wiki ya mwisho ya mwezi kwa siku ya Jumamosi, maana mazoezi ni afya. Ingawa Mheshimiwa Waziri Ummy anajitahidi kuhamasisha Watanzania lakini binadamu ni mzito. Hata sisi baadhi yetu Wabunge endeleeni kutuhamasisha kwa kufanya mazoezi kwa baadhi yetu tayari tunasumbuliwa na pressure pamoja na sukari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la watoto njiti. Nursing ya watoto njiti ni mtihani kwani hakuna uangalifu na watoto wanafariki kwa kukosa matunzo. Vifo vya akina mama, vifo vya watoto hivi sasa kati ya akina mama 100,000 basi kuna akina mama 430 hadi 556 hufa kwa uzazi kwa kukosa huduma. Ninajua Waziri wa Afya ni mwanamke na ninajua atachukua hatua za haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kukosa theatre kwa ajili ya akina mama kujifungulia kwani mama anatakiwa kuwa karibu na sehemu ya kujifungulia. Ingawa Wizara yako ilitakiwa kutekeleza; je, suala hilo limefikia wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.