Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Kagera ni mojawapo ya Mkoa wenye upungufu mkubwa wa Madaktari. Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, wanahitajika Madaktari (MD) 30; waliopo ni 12, pungufu ni 19. Madaktari Bingwa wanaohitajika ni 24 ila wapo watatu. Daktari Bingwa wa magojwa ya akinamama, Daktari Bingwa wa meno na Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia upungufu huo, Mkoa uliamua kuajiri Madaktari (MD) na kuwalipa kwa kutumia fedha za uchangiaji wa huduma za afya (cost sharing). Hadi wiki iliyopita, walikuwepo Madaktari (MD) saba ambao wanalipwa kwa fedha za cost sharing. Madaktari hao ni Dkt. Yunus H. Ibrahim; Dkt. Nathaniel Ngeta, ambaye kwa sasa amepelekwa kwa DED Kyrerwa; Dkt. Paschal Peter; Dkt. Goodluck Chenga, kwa sasa amepangiwa Hospitali ya Mkoa Bukoba; Dkt. Bartazar W. Benedicto, amepangiwa Wizara ya Afya; Dkt. Lunyonga R. Shija ambaye kwa sasa amepangiwa Hospitali ya Mkoa Bukoba; na Dkt. Felix T. Otieno ambaye kwa sasa amepangiwa Hospitali ya Mkoa Bukoba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Madaktari hao wawili waliobaki wapewe kipaumbele cha ajira na wapangiwe kufanya kazi kwa RAS Kagera. Pia tunaomba Madaktari Bingwa zaidi ili kupunguza upungufu uliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maombi ya vifaa vya uchunguzi hasa CT-Scan na MRI pamoja na wataalam wa kuvitumia vifaa hivi vya uchunguzi ni muhimu kwa Hospitali ya Mkoa, kwa sababu huduma hii ya uchunguzi inapatikana Mwanza. Hivyo tunaomba sana muweze kutukumbuka Mkoa wa Kagera. Pamoja na maombi hayo, tunaomba pia Halmashauri zetu zipewe kipaumbele katika mgawo wa Medical Doctors (MD) hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya Halmashauri tayari zimeanza kutoa huduma ya upasuaji CEMONC katika vituo vya afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vituo vinavyotoa huduma ya upasuaji, licha ya upungufu wa Madaktari ni Nyakachura na Nyakanazi katika Halmashauri ya Wilaya Biharamulo; pia kwenda katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa na Kayanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe. Vituo vinne vya afya vinavyotarajiwa kuanza kutoa huduma za upasuaji kupitia Mpango wa Strengthening Primary Health Care for Results Programme ni Mabame (Ngara), Kimaya (Muleba), Kishanje (Bukoba) na Morongo (Kyerwa). Vituo vingine vilivyokamilisha ujenzi wa theatre ili kuanza kutoa huduma za CEMONC ni Kaigara (Muleba), Bunazi (Missenyi), pamoja na Kabyaile (Missenyi) kilichojengwa na Kamati ya Maafa kufuatia tetemeko la ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.