Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi sasa ya kuchangia baada ya kususia hotuba kutokana na kubanwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze sijui na Mwenyekiti, sijui Katibu, ni Naibu Katibu, Kiongozi Mstaafu wa UVCCM anayesema kwamba tukiudharau mwenge tutapata taabu sana. Ninyi mmemdharau Mwalimu Nyerere na bado mna- survive, itakuwa sisi kuudharau mwenge! Mmedharau misingi mingi sana ya Mwalimu Nyerere ambayo aliiweka katika nchi hii. Mnalinda mwenge badala ya kulinda Azimio la Arusha ambalo lilikuwa na misingi mizuri kabisa kwa ajili ya kuwa na viongozi bora wa nchi hii. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna mtu anayesimama kwenye Bunge hili, hata wewe uliyekuwa kiongozi wa UVCCM, sijawahi kusikia hata siku moja unamkumbuka Seth Benjamin, shahidi wa Azimio la Arusha. Mnatetea vitu vyepesi vyepesi tu, mnasimama humu ndani. Unasema lazima tukimbize mwenge kwa sababu upo kwenye ngao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye ile ngao kuna jembe na nyundo na pembe ya ndovu. Sasa tuvichengue vyote kuwe na route ya pembe, jembe na kuwe na route ya shoka nazo viwe na mbio zake kwa sababu tu zenyewe nazo zipo kwenye Ngao ya Taifa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, alichokizungumza Mheshimiwa Lissu ni kitu cha msingi sana. Nembo za Taifa zinaeleweka na tunatakiwa tuziheshimu, tusipotoshe kama tulivyopotosha mambo mengine huko nyuma. (Makofi)

Mhesimiwa Mwenyekiti, huu mwenge ndiyo maana hata sijauzungumzia kwenye hotuba yangu, hauna hata shughuli ya kufanya; wanavizia miradi. Mbeya Mjini mathalani toka uhuru kulikuwa hakujajengwa madaraja yanayounganisha Jiji la Mbeya na kata za pembezoni kuelekea Mbeya Vijijini, kunazunguka mto. Leo hii chini ya Meya wa CHADEMA, Mheshimiwa Mwashilindi katika kipindi kisichozidi miaka miwili, tumejenga zaidi ya madaraja kumi kuunganisha Jiji la Mbeya na pembezoni. Huko nyuma chini ya Meya wenu hamkujenga, sisi tumejenga halafu eti mnakuja kuleta mwenge kuzindua, ndiyo maana wananchi hawakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sisi humu ndani pia tunawakilisha wananchi, hatuwezi kuja humu ndani kuzungumza kitu ambacho ni unpopular huko nje. Only people ambao wanaweza kufanya hivyo ni ninyi kwa sababu mnazozijua wenyewe. Mnajua kabisa hiki kitu hakitakiwi na wananchi, lakini mna-impose, mnalazimisha. That is you, sisi hatutafanya hivyo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wasanii, ifike sehemu sasa sisi wasanii tuache kutumika. Unaangalia move kama ya hawa watu wa filamu ya hivi karibuni, wanaitwa na Bashite. Bashite kakataliwa na jamii zote, mpaka masela wa hip hop wamemkataa, washikaji zake ambao alikuwa nao anafanya naye gym huwaoni tena, wamemkimbia; ameenda kuchukua wanyonge wa bongo filamu, anawakumbatia, anatoa matamko ya ajabu baada ya kukataliwa na vyombo vya habari (media). Wasanii tunaachaje ku-support vyombo vya habari wakati ni wadau wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vyombo vya habari ni wadau wetu. Bila wao sisi hatuwezi kufanya sanaa. Ukiona wapo katika movement fulani kudhibiti kitu fulani chenye manufaa kwa nchi, ni lazima sisi wasanii tuunge mkono wanahabari. Wanahabari wamemsusia Bashite, sisi tunaenda tu kukaa pale kwenye makochi ya Serikali kumsaidia kujisafisha na kumnasua. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema wanasiasa tuache kutumia wasanii vibaya, tuache ku-abuse wasanii. Mpaka Wabunge, juzi anasimama humu Mheshimiwa Keissy, huwa na namwita mzee, lakini simwiti mzee, anasimama anasema Msanii Roma kamtukana Rais. Hamjui hata Roma, hajawahi kumwona. Kwanza yeye ni sala tano anavyotuambia, anajuaje mambo ya hip-hop? Hamjui Roma, hajawahi kumwona, anatoka anasema, Roma kamtukana Rais. Wapi? (Kicheko)

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mwakyembe ulienda kukaa na mtu aliyemtukana Rais wako pale kwenye press? Halafu watu mnapiga makofi, mnashangilia. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema, mtu kama Mheshimiwa Keissy nampuuza. Kwanza Bunge lililopita miaka mitano yote alikuwa anatetea bangi humu ndani; nashangaa hajaulizwa. Miaka mitano yote alikuwa anatetea bangi. Alinifuata mimi, bwana tutetee hoja ya bangi; nikamwambia bwana, mimi hayo mambo siyajui, wala sijawahi kuyagusa. Utajijua mwenyewe huko. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi namtaka Roma Mkatoliki, msanii wa muziki ambao nimeuasisi, atoke sasa aongee kwa uwazi, in details kilichomkuta ni nini? Public ikishajua, inaweza ikasaidia kujua ni nani waliomteka yeye na wenzake na walitumwa na nani, full stop. Vinginevyo tutaendelea kuwa na debate kama za Ben Saanane hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ripoti ya Nape, naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kujibu atuambie kabisa kiuweledi what made you deny ripoti ya Waziri aliyekutangulia Mheshimiwa Nape? Huyu mtu Bashite ameenda kuvamia kituo cha redio na tv mpaka studio na watu wana bunduki, machineries, polisi wamesema hawawajui wale watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nani wale watu walioenda kuvamia kituo cha Clouds fm? Kuna watu wananiambia, Sugu ulikuwa na bifu na Clouds miaka yote, sasa hivi unawatetea. Nilikuwa na bifu na Clouds kwa sababu ya haki. Haki ni haki, iwe dhidi yangu, iwe ni dhidi ya Clouds na mtu yeyote, nitatetea. Hata kama ninyi huko nikiona Waziri yeyote hatendewi haki, nitamtetea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu mtu ripoti imewekwa wazi kwamba amefanya makosa, kwa nini analindwa? Analindwa kwa maagizo ya nani Bashite? Maagizo ya nani yanafanya eti waseme hatuwezi kuchukua hatua kwa sababu Bashite hakusikilizwa? Hakusikilizwa wakati Tume imeenda imekaa ofisini kwake masaa matano, sita, saba, nane, akatokea mlango wa uani! Sasa yeye ni bingwa wa kuwaambia watu tukutane central police, tukutane mahakamani; yeye anaitwa kwenye vyombo halali vya sheria, chombo kilichoundwa na Waziri, anaingia mitini, he is a coward.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bashite is a coward, ni jambazi, thug, ni criminal ni fraud. Bashite ni fraud kwa sababu ame-forge vyeti. Halafu Serikali inatoka inasema ooh, hatukuwagusa wanasiasa. Ma-RC na ma-DC siyo wawakilishi wa wananchi. Sisi hapa ndiyo tunaweza kuingia kwenye uongozi kwa kusoma na kuandika, lakini siyo RC wala DC. Wale wanatakiwa lazima wawe na level fulani ya elimu na hili suala linajulikana wazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi, suala la Bashite siyo kwamba ana elimu gani? Suala ni ku-forge. He is a fraud! Amefanya forgery, anatakiwa kusimama mahakamani, ndipo sehemu anapotakiwa kusimama. Sasa kinachomfanya azuiwe asichukuliwe hatua hizo …

KUHUSU UTARATIBU....

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sasa Serikali kupitia Waziri wa TAMISEMI inaanza kutupa mwanga wa Bashite ni nani, kwa sababu inaleta mjadala sana katika Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, huyu mtu ni fraud. Tunaonea watu wadogo, watu wanalazwa, watu wanazimika, eti nchi hii wanasema dereva wa Mkuu wa Mkoa anatakiwa awe na cheti cha form four, lakini Mkuu wa Mkoa hata kama ameishia darasa la pili, akiweza kusoma na
kuandika that is a big joke! Ilibidi mje na maelezo yanayonyooka. Tanzania hii nawaambia kila siku, watu wameamka, siyo kama Tanzania ile ya zamani unaamka tu unasema kwamba kiongozi fulani fikra zake zimeota; ameota au amefanya nini ndiyo maono sahihi kwa asilimia mia moja. Hata wakati huo, kulikuwa na mijadala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge la wakati ule mimi nikiwa mdogo, tulikuwa hatuoni kwenye tv, tunasikiliza kwenye redio, kuna watu walikuwa wanaitwa akina Tuntemeke Sanga na Mohamed Nandonde, huwaoni kwa sura lakini lazima usikilize Bunge ukisia kwamba anadai barabara ya Mtwara wakati ule. Halafu sasa hivi mnakuja mnasema tu tumefanya hivi, tumefanya hivi, mnasahau watu waliofanya kazi, mnamsahau Rashid Kawawa na Mwalimu Nyerere. Hata mtoto wa Kawawa juzi mmemnyima Ubunge hapa wa Afrika Mashariki, halafu mnajidai mnaenzi watu. Mtoto wa Nyerere pia mmemnyima Ubunge wa East Africa hapa, halafu mnasema mnaenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii cybercrime naona imeanzishwa kwa ajili ya UKAWA tu. Wakati vijana wa UKAWA kutoka akina Mdude Nyagali kutoka Mbozi mpaka hao tunaozuiwa tusiwataje, akina Ben Saanane wanapata matatizo, wanakamatwa na kunyanyaswa kwa kutoa maoni yao kwenye mitandao, vijana wa CCM wanatukana Viongozi wa Upinzani mpaka matusi ya nguoni lakini hakuna mtu ambaye anawakamata wala kuwachukulia hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitu hivi mnaweza mkaona ni vitu vyepesi sana, lakini niwambieni mna… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.