Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza sina budi kumshukuru au kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa umahiri wake anaouonesha Tanzania kuimarisha uchumi, uwajibikaji na maendeleo katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile sina budi kumshukuru Makamu wa Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, mama chapa kazi na tunakuona umevaa viatu vya Marehemu Dkt. Omar Ali Juma, umevaa viatu vya Dkt. Mohamed Shein,

tunakuona unavyoenda mbio na Muungano na Muungano utadumu. Mama unapofika Dodoma mwezi wa Ramadhani, usitusahau katika ufalme wako, Inshallah. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie Ziwani Zanzibar katika Jimbo la Jang’ombe. Ziwani marehemu bibi zetu tulikuwa tunasikia wanaita Bomani. Mimi nazaliwa nimeliona Ziwani boma liko vilevile na mpaka leo liko vilevile, kama linatengenezwa matengenezo yake siyo makubwa. Isitoshe unapotaka kuingia bomani njia za panya zimejaa tele, ukaingia ndani na utatoka hakuna atakayekuona ingawa wao wenyewewanatumia milango, kuna milango mizuri na kuna ulinzi, lakini imekuwa ni bure wakati milango iko ya kuingilia na kutoka na humu kuna milango ya panya imekuwa haina maana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema hivyo kwa sababu ya uzio, uzio uliojengwa toka ukoloni mpaka leo haujatengenezwa, Ziwa liko karibu na mitaa wanayokaa watu, wametengeneza njia za panya. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri aende akaangalie na aweze kutuwekea imara ya boma letu ambalo tunaliamini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia vijana wetu hawa ambao katika ukurasa wako wa 11, Mheshimiwa Waziri alizungumza udhibiti wa dawa za kulevya. Najua dawa za kulevya nikizungumzia ‘unga’ haliko kwenu, kuna kitengo kimeundwa, lakini nalileta kwenu kwa sababu mnao askari wa kutosha wa kusaidia kitengo kilichoundwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, marehemu bibi yangu niliwahi kumsikia akizungumza kuna Askari Kanzu ambao niCID. Hawa askari kama mtawatumia wataweza kukisaidia hiki kitengo, kwa sababu hiki kitengo kinahitaji kipate watu na ninyi ndiyo mtakaoweza kuyapangua haya mafiga matatu, kwa sababu kuna mletaji, kuna msambazaji na kuna mlaji. Sasa hawa wote, hili figa hili kama hamkuweza ninyi kuliangalia mkalipangua kwa sababu CID anaweza kupenya sehemu zote akampata mletaji, akampata msambazaji, walaji tunawaona kwa sababu picha yao inaonekana, ili muweze kukisaidia hiki kitengo tuweze kusaidia nguvu kazi ambayo inapotea katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu suala la NIDA. Unajua katika bajeti yenu ya mwaka jana, mlizungumza kwamba hiki kitengo mtakiboresha baada ya kupata vifaa kutoka Tume ya Uchaguzi. Vifaa mmevipata, lakini hakuna kinachotendeka. Hatuoni tena NIDA kazi inayoifanya, hatuoni kuangalia kuboresha maslahi ya watu, wafanyakazi waNIDA mmewatoa/mmewapunguza, sasa kweli hivi vifaa mlivyopewa vikae ndani ni mapambo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vifaa vilivyopo mle ndani viweze kufanya kazi na wafanyakazi ni hawa vijana ambao tayari mmewatoa. Maana mmesema mtafanya utambuzi wa Watanzania, mtafanya usajili wa Watanzania, usajili hauko, upembuzi hauko, watu wanajiingilia na kutoka. Nataka Waziri utakapokuja uniambie, kwa nini mlipunguza wafanyakazi na wakati ulikuwa hujaimaliza kazi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.