Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizari ya Maji na Umwagiliaji

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizari ya Maji na Umwagiliaji

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Na mimi nachukua fursa hii kwanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri na menejimenti yote ya Wizara, kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya. Maana tukisema kwamba hawafanyi kazi vitu vingine vinakuwa siyo katika disposal yao kwa hivyo nadhani hapa tulipo wamejitahidi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye sekta ya maji changamoto zipo nyingi, kuna kurasa ambazo Mheshimiwa Waziri amendika, kurasa 128, 129 na 130 anapongeza zile taasisi za kimataifa na mashirika pamoja na NGO’s ambazo zinasaidia sekta ya maji, ni nyingi kweli. Mimi nadhani tukiangalia kwenye assessment, sekta ambayo inapata support kutoka mashirika ya nje na ya ndani ni sekta ya maji, tuna karibu mashirika 62.

Hata hivyo, tukiangalia fedha ambazo zimepatikana katika kipindi cha bajeti ambayo tunakamilisha mpaka Machi ni fedha ndogo sana shilingi bilioni 181 ambayo ni sawa na asilimia 19 lakini wachangiaji wako wengi kweli. Hapa sasa lazima tujikite katika kuhakikisha kwamba tunaweka mikakati ya kuona kwamba fedha zetu sisi wenyewe za ndani ndizo zitakazokwenda ku-finance sekta ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, issue hapa wala siyo kuongeza bajeti, maana ukisema unakwenda kuongeza bajeti you just increase the numbers and then what? Hakuna hela, it is not about Hazina atoe hela, Hazina hana hela ni lazima aende akazitafute. Kwa hiyo, lazima tutafute chanzo ambacho kitakuwa sustainable ili kuweza kuona kwamba maji yanapatikana. Shilingi 50 kwa mimi ninavyoona tumepata shilingi bilioni 95 ambayo imekwenda kusaidia kwa kiasi kikubwa, tuongeze shilingi50 nyingine kwenye lita hizo za mafuta. Hata hivyo, tunaweza tukaenda further tukaangalia vyanzo vingine, zile products ambazo zinatokana na maji zinaweza zikatozwa kwa asilimia fulani hata shilingi mbili kwa kila lita ili kusaidia kwenye Mfuko wa Maji, mimi nadhani hatua hiyo inaweza ikatusogeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya maji ina changamoto kubwa na ni sekta ambayo inategemewa karibu na kila sekta nyingine kwa mfano afya, elimu, ujenzi, kilimo na utalii. Sekta hii yenyewe ni lazima iweze kupeleka huduma katika sekta nyingine, hizi sekta nyingine zenyewe haziwezi kusaidia katika sekta ya maji. Kwa hiyo, tunaona kwamba hii ni changamoto na hapa tunaweza tukamsema Waziri, wewe Waziri sijui kizee, sijui nini, no, it is not about that, hii ni changamoto ya Taifa. Kila mtu anasimama labda anamshambulia Waziri, hii siyo katika disposal yake. Kwa hiyo, wakati tunachangia ni lazima tuone tunaisaidia vipi Serikali kupata chanzo cha fedha ambacho ni endelevu, kiko reliable kuweza kusaidia sekta ya maji. Shilingi bilioni 95 zilizopatikana kutokana na shilingi 50 ni asilimia 53 ya fedha ambazo imetolewa, ni hatua kubwa. Kwa hiyo, tukiongeza na nyingine nadhani Mheshimiwa Waziri tutakapokuja hapa mwaka kesho tukifanya tathmini ya sekta ya maji nadhani tutakuwa tumepata mafanikio. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kubwa zaidi lakini siyo kwa umuhimu kwamba nalisema mwisho kwa sababu ya muda, Mheshimiwa Waziri utakapokuja lazima utueleze fedha zinazotoka Exim Bank ya India ambazo mwaka jana ulizisema kwa mbwembwe zote na sisi Wabunge tunaotoka Zanzibar tulishangilia kweli, tukafanya kikao kuzipangia matumizi. Leo hatujaona kitu chochote, 31 million dollors, ni fedha nyingi sana na zinaweza zikabadilisha hali ya maji kule Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimboni kwangu tulitegemea sana fedha hizi mwaka huu ziende zikarekebishe miundombinu ambayo imechakaa mno na tuna dhiki kubwa ya maji, lakini safari hii naona hatujakusikia. Nadhani umesoma a line one or two lakini hatujajua process hii imefikia wapi, tunataka utupe maelezo ya kina. Tunajua kwamba masuala ya mobilization siyo yako, lakini kwa sababu umelizungumza Mheshimiwa Waziri ni lazima ulitolee majibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na naunga mkono hoja.