Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Nina jambo moja. WMA ni sehemu ya ardhi ya vijiji kwa maana kwamba Serikali za Vijiji na wananchi wao walikaa wakatoa hayo maeneo wakaunda WMA ili wanyamapori wakiingia humo wao wawekeze wapate mapato. Ni vizuri Waziri afahamu sera na sheria iliyoanzisha WMA ilikusudia nini, ilitaka kugatua madaraka kuyapeleka kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa WMA zimeundwa lakini mmeanza kuziua kwa kuanzisha kitu kinaitwa single entry. Ikona WMA ambayo ndio WMA kioo ambayo ina-shine kuliko WMA zote, mmeiua. Camps zote na hoteli zilizokuwa zimewekeza kwenye ile WMA wameanza kuondoka kwa kukosa wageni. Mwaivaro ni camp ambayo ilikuwa inapata wageni 400 kwa msimu sasa hivi wameshuka mpaka 70. Camps nyingi pale zimeondoka kwa sababu ya issue ya single entry. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri Mheshimiwa Waziri afahamu kwamba ili uende Ikona WMA lazima utokee Arusha na ukitokea Arusha lazima u-cross Serengeti National Park, kwa ku-introduce mfumo wa single entry wageni hawaendi tena Ikona WMA, you kill it. Sisi tunasema ahsante, yeye aue tu lakini kwenye ardhi ile sisi tutafuga ng’ombe na tutalima tumbaku kwa sababu hawataki sisi tufanye conservation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamekuja hapa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji wa maeneo yanayounda Ikona WMA, wamekuja Madiwani na wajumbe wa WMA tukaenda mpaka kwa Mheshimiwa Waziri akasema ataishughulikia hii ya Serengeti ni very unique, baadaye akaniambia Kamati imekataa. Mimi nikachukua jukumu la kwenda kwenye Kamati ya Maliasili na Utalii hata hawana habari, sasa ni Kamati ipi ilikataa? Sasa mimi nataka leo kwa dakika hizi tatu ambazo nimepewa atakapokuja ku-wind-up aniambie yuko tayari kuangalia upya mfumo huu wa single entry au wapo tayari kuua hizi WMA?

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. MARWA R. CHACHA: Kama msipopitia upya kanuni hizi zilizounda WMA, you will kill it na sisi hatuna shida tutachunga tu ng’ombe mle.