Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia katika Wizara hii hasa eneo la ubora wa zana za ufundishaji hasa vitabu vya kiada. Tangu Serikali ilipovunja Bodi ya EMAC uhakika wa vitabu umekuwa dhaifu sana na kusababisha upotoshaji mkubwa kwenye taaluma, hivyo kuchochea Taifa kudondokea katika umbumbumbu, ujinga na kukosa maarifa kwa watoto wetu. Vitabu vilivyopo sasa ni ushahidi wa dhahiri kuwa uwepo wa EMAC usingeweza kupitisha makosa haya. Pia dhamira ya kuirejesha EMAC iendane na suala zima la kuihusisha sekta binafsi ifanye kazi hiyo na Serikali ibaki kuwa mthibitishaji ili hata makosa kama haya yakijitokeza yasiiathiri moja kwa moja Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kukuza uwekezaji katika viwanda. Serikali inapoamua kuchapa vitabu yenyewe sio lengo baya, lakini inakinzana na sera ya viwanda. Aidha, uwepo wa sekta binafsi katika tasnia ya uchapishaji itasaidia Serikali kuyaona mambo kwa jicho la mbali na jicho pana zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niweke ushahidi wa vitabu vifuatavyo kuonyesha makosa ya dhahiri na ya wazi katika uchapishaji kuonyesha udhaifu mkubwa wa Taasisi ya Elimu kusimamia tasnia hii ya ukuzaji maarifa na utoaji elimu kwa vijana wetu.

(i) English For Secondary Schools, Form Four – ISBN 978- 9976-61-460-2

(ii) Geography for Secondary Schools, Form Three - TIE of 2016 –ISBN 978-9976-61-479-4

(iii) I learn English Language, Standard Three – ISBN 978- 996-61-545-6. (Vipo ikiwa ni ushahidi wa dhahiri).

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo yote yenye makosa yameainishwa na kuwekewe alama maalum kwa (highlighter).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha, ahsante.