Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kuhusu hali ya usalama nchini. Kwa sasa hivi unaweza kusema kuna utulivu tu; kwa sababu tumeshuhudia siku za hivi karibuni pamekuwepo na matukio mengi sana ya watu kuuawa bila sababu, kwa mfano askari waliouawa huko Kisarawe kwa kupigwa risasa na watu wasiojulikana, matukio kama haya yametokea Pangani na Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali imeshafanya uchunguzi wahusika ni akina nani? Watu hawa wanaweza kuanza taratibu uhalifu huu kwa kuanzia pembezoni mpaka wakafika mjini, tutakuwa tumechelewa, je, Serikali inawaeleza nini Watanzania kuhusu matukio haya yanayotishia usalama wa Watanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Jeshi hili linajishughulisha na kazi za maendeleo kupitia vikosi vyake kama ujenzi wa barabara, mpaka gari wamewahi kuunda, na kwa kupitia Jeshi hili tunaweza kuokoa fedha nyingi sana hata kuwapa tender za samani za ofisi za Serikali kama walivyotengeneza madawati, nawapongeza sana. Hata hivyo changamoto kubwa ni utolewaji wa fedha za maendeleo ndiyo unawakwamisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano waliomba shilingi 248,000,000,000/= kwa ajili ya maendeleo lakini wamepata shilingi 35,000,000,000/=, sawa na asilimia 14.5 ya bajeti waliyoomba. Je, kwa ufinyu huu unaotolewa wataweza kutimiza majukumu yao? Hii ni kuwarudisha nyuma, badala ya kuendelea wamebakiwa na kulipa madeni. Tukumbuke Jeshi hili kwa sasa ndilo linalotusaidia kuwajenga vijana wetu kimaadili kwa kwenda jeshini, wale wanaomaliza kidato cha sita. Je mpaka sasa hivi Serikali imeweza kuchukua vijana wangapi kwenda jeshini?