Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika hotuba hii. Nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha hotuba hii na kuiwasilisha kwa utaalam mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mikopo ya Pembejeo; napenda kuipongeza Serikali yetu kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwapatia mikopo wakulima wetu. Wakulima wetu ni wa kipato cha chini sana (maskini), hivyo ni nyema kuwapatia mikopo hii. Naiomba Serikali izidishe jitihada ya kuwapatia mikopo na kuwawekea mazingira rafiki wakulima wetu ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hali ya Uvuvi; sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi na wananchi wetu. Hivyo ni vyema Serikali yetu ikachukua juhudi za makusudi katika mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwaendeleza wavuvi wadogo, kuwapatia elimu na kuwapatia vifaa vya kisasa. Serikali ni lazima ichukue na iwe na mpango maalum wa kuwaendeleza na kuwapatia elimu wavuvi wadogo. Wavuvi wetu wanajitahidi sana lakini bado hawana mwelekeo, bado wanafanya kazi ya uvuvi kwa mazoea. Ni vyema Serikali iwapatie elimu na miongozo juu ya kujiendeleza. Aidha, Serikali iwapatie vifaa vya kisasa vya uvuvi. Hivi sasa vifaa ambavyo wavuvi wetu wanavitumia bado ni vya kizamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.