Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Jang'ombe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, Msajili wa Hazina Fungu Na. 7, kuziongezea uwezo taasisi zilizo chini ya Msajili wa Hazina kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, NARCO, taasisi hii ingeongezewa uwezo wa kuwa na ranchi nyingi katika maeneo ambayo yana mifugo mingi. Pia taasisi iweze kutoa taaluma kwa wafugaji wa wanyama wa asili ili mifugo yao iwe na tija.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Tanzania ni ya pili/ tatu kwa mifugo Barani Afrika lakini pia ni nchi yenye migogoro ya wakulima na wafugaji, hivyo basi tutumie changamoto na uimara huu kupitia ranchi zilizo chini ya NARCO kuweka hali sawa. Pia taasisi hii ingepewa uwezo zaidi wa kuzalisha mitambo ya maziwa
Mheshimiwa Mwenyekiti, TANAPA; Tanzania ni ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vya utalii baada ya Brazil. Hivyo, taasisi hii iwezeshwe zaidi katika mambo yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, iongezewe uwezo wa kujenga miundombinu ili vivutio hivyo viwe vinafikika na watalii wa ndani na nje pia kujenga uwezo wa kuweza kuvitangaza vivutio hivyo ili kupata watalii wengi kwani uchumi tunao lakini tunaukalia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, COSTECH; (Taasisi ya Utafiti) kwa uchumi wa viwanda, tuwekeze zaidi katika kufanya utafiti hasa kwa kuwatia moyo wabunifu. Income from Investment pia Serikali iwekeze zaidi katika mashirika yanayofanya vizuri ili tuweze kupata pato kutoka kwenye uwekezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Takwimu; Tunakwenda katika uchumi wa viwanda, lakini mpaka sasa kuna upotoshwaji wa takwimu kama vile sukari inayohitajika kwa matumizi ya ndani ya nchi, hivyo imepelekea kupata upungufu wa sukari na bei ikapanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuhusiana na uamuzi wa kuzidisha mwaka 2016/2017 asilimia 10 kwenye mafuta ghafi hatimaye bei imepanda na tunatumia mafuta hayo kutoka nchi jirani kwa magendo kutokana na kukosa takwimu sahihi. Ofisi ya Takwimu ipo wapi? Kwa nini hatuna takwimu sahihi? Kwa nini tunatumia takwimu za wafanyabiashara badala ya kutumia takwimu toka Ofisi ya Takwimu tukaacha kupotoshwa? Izingatiwe kwamba wafanyabiashara hawa wapo makundi mawili kila kundi linataka kuangusha mwenzake.