Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii adimu sana. Naungana na Waheshimiwa Wabunge kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu wake na Watendaji wote wa Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siri kubwa ya mafanikio ya Wizara hii, wanasikiliza tatizo, wanakwenda site, wanalishughulikia na wanaweka mifumo ya kuhakikisha kwamba tatizo halijirudii. Hongera sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri spirit aliyotumia ya kuweza kutatua migogoro maeneo mbalimbali, aje Kaliua akishirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii atatue migogoro ambayo inawasumbua wananchi wa Kaliua kwa muda mrefu na kuondokana na mateso na maumivu wanayopata wananchi wa Kaliua kwa sababu ya migogoro ya ardhi ya kati ya wananchi na hifadhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni la upimaji wa ardhi. Speed ya kupima ardhi bado ni ndogo, asilimia 25 ni ndogo sana. Tunatamani kwamba mwananchi anapohitaji ardhi aweze kupewa kiwanja ambacho tayari kimepimwa. Kwa hiyo, naomba sana kwenye Mfuko wa Kupima Ardhi lazima kuhakikisha kwamba kuna fedha ya kutosha. Iwepo fedha ya kutosha na vifaa vya kupima ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Ardhi imeweka kipengele kwamba Waziri atatenga eneo la mifugo; eneo litapimwa, litakuwa gazetted na pia litalindwa. Kwa hiyo, naomba wakati wa kupima ardhi kwenye maeneo mbalimbali, Mheshimiwa Waziri ahakikishe anatenga maeneo ya mifugo na pia maeneo yawe gazetted na yaweze kulindwa. Ndiyo inayosababisha migogoro mikubwa sana ndani ya nchi yetu kutokana na migogoro ya ardhi kwa wakulima na wafugaji na hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine naomba ahadi ya National Housing; pamoja na kazi nzuri wanayoifanya, wafike Kaliua. Ni Wilaya ambayo ni mpya, lakini inakwenda speed sana kwa maendeleo, waje wawekeze ndani ya Wilaya ya Kaliua, kujenga nyumba nzuri nasi tuweze kuwa wa kisasa kama ambavyo Wilaya nyingine wameweza kujengewa nyumba na National Housing.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, hawa watu wa Mfuko wa Kujenga Nyumba za Watumishi (Utumishi Housing), usambae uende maeneo mengi, ufike mpaka Kaliua. Watumishi wetu hawana nyumba, wamepanga nyumba ndogo ndogo za vijijini huko. Tunaomba na wenyewe waje Kaliua wapanuke katika maeneo mengi; sasa hivi wame- concentrate kwenye maeneo machache sana. Mfuko uongezwe ili watumishi wetu wa maeneo mengi waweze kupata nyumba za watumishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine. Migogoro mikubwa ya ardhi inasababishwa na uelewa mdogo pia wa Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Mheshimiwa Waziri atoe elimu kwa Viongozi wa Vijiji. Viongozi wa Vijiji wanatoa maeneo makubwa sana. Sheria inaruhusu ukomo wa kutoa eneo la kijiji, lakini wanatoa mpaka hekta 1,000 au 2,000 na wanapokea rushwa, wanaleta watu bila hata wananchi kujua. Kwa hiyo, naomba itumike busara viongozi wapewe semina na mafunzo waweze kutumia Sheria ya Ardhi kugawa maeneo ndani ya vijiji vyao ili kuondokana na migogoro inayosababishwa na kugawa ardhi bila kufuata Sheria ya Ardhi.