Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kodi ya Ardhi, maelekezo yalitoka kwenye hotuba ya ardhi kwamba wananchi wote wanaomiliki ardhi iwe imepimwa au haijapimwa lazima walipe kodi, sasa ardhi hiyo ambayo haijasajiliwa kisheria italipiwaje kodi? Je akilipia kodi ataweza kutumia receipt hiyo kwa ajili ya dhamana yoyote? Serikali ifuate sheria ndiyo maana tulizitunga ambapo wananchi hulipa kodi kwenye ardhi iliyopimwa tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba (NHC), Shirika hili limekuwa likifanya kazi nzuri kujenga nyumba za biashara na makazi lakini madhumuni ya kuanzisha NHC yalikuwa ni pamoja na kujenga nyumba za bei nafuu ili kila Mtanzania aweze kuishi kwenye nyumba kwa haki. NHC imeshindwa kujenga nyumba kwa bei nafuu kutokana na vifaa vya ujenzi kuwa na bei ya juu sana na kupelekea ujenzi kugharimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwasaidia wanyonge, lakini kwa mtindo huu wa bei za nyumba wanazoziita ni za bei nafuu za milioni 60 ni mfanyakazi/Mmachinga yupi wa kawaida atakayeweza kulipia bei hiyo? Ushauri, Serikali ishushe kodi kwenye vifaa vya ujenzi kwa nyumba zinazojengwa na NHC ili waweze kuendeleza kazi nzuri wanayojitahidi kuifanya kwa ajili ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhaba wa vitendea kazi na wataalam, pamekuwepo na uhaba mkubwa wa vitendea kazi na wataalam kwenye kitengo cha kupima ardhi ambako kunapelekea wananchi kwenda kutumia wapima ardhi binafsi na wanatoza pesa nyingi ambapo inapelekea wananchi wengi kutopima ardhi zao. Serikali inapoteza fedha nyingi kwa kutopokea kodi ya ardhi. Je, Serikali imetenga fedha kiasi gani kwa ajili ya vifaa kwa nchi nzima ikiwa ni pamoja na kuajiri wataalam wa kutosha kwa nchi nzima? Mfano pale Moshi Vijijini (Wilaya ya Moshi) hawana vitendea kazi kabisa hata usafiri haupo. Ni kwa nini hata kwa kuanzia wasiwe hata na pikipiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napenda nimpongeze Waziri, Naibu Waziri na Watumishi wote wa Wizara kwa kazi nzuri wanayofanya kwa kujaribu kupunguza migogoro ya ardhi. Nawashauri mjaribu kutatua matatizo yaliyobaki kuna uhaba wa wataalam na vifaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mategemeo yangu watachukua maoni ya Upinzani na wayafanyie kazi kwa faida na maendeleo ya nchi yetu na wananchi wetu.