Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nami nawashukuru Wenyeviti wote wa Kamati waliowasilisha, lakini na mimi najikita zaidi kwenye Wizara ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sisi wengine tuliotoka Bunge liliopita na wakati ule Bunge la Tisa tulipokuwa tukiangalia kwenye television, Bunge kama hili lilikuwa Bunge lenye uhai, Bunge ambalo Serikali inasikiliza hoja ambazo baada ya Waheshimiwa Wabunge kutembea maeneo mbalimbali wanajaribu kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni tofauti sana na Bunge hili ambalo kwa kweli limepooza, unakuta hata Kiongozi Mkuu wa Serikali hayupo hapa, Wabunge wanajaribu kutoa maoni yao na kuishauri Serikali, Mawaziri wanachelewa kama hivi Mheshimiwa Waziri wa Maliasili ni hoja yake hapa, ndio anafika saa hizi. Kwa hiyo, hizi ni hoja ambazo tunakiwa tujitathmini kama kweli Bunge tunatimiza majukumu yetu. (Makofi)

T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo taarifa siipokei. Labda ni Awamu ya Tano ndiyo utaratibu wake. Nimezungumza Bunge la nyakati za nyuma, Spika akiwa Marehemu Mheshimiwa Sitta au Mheshimiwa Anna Makinda, tulikuwa tunamwona Waziri Mkuu anakuwa hapa, tunampa taarifa jinsi tunavyofanya kazi huko. Utaratibu wa sasa hivi toka Bunge limeanza Waziri Mkuu hayupo, Mawaziri wenyewe wanakuwa hawapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu ndiyo hiyo, Serikali haitilii maanani hoja ambazo sisi kama Wabunge tunataka kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachonisumbua ni jinsi ambavyo haya mambo tumekuwa tukitoa ushauri miaka nenda rudi, lakini tunarudia kila mwaka kuyazungumza yale yale. Kamati ya Maliasili katika kitabu chao ukurasa wa 33, wamesema, Kamati ilikutana na Mkutano wa Wadau na Uwindaji wa Kitalii nchini na kupokea malalamiko yao kuhusu hatua ya Waziri ya Maliasili na Utalii kufuta leseni zote za umilikaji vitalu kwa kipindi cha miaka 2018 na 2022. Sitaki niendelee sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, industry hii ya uwindaji kwa muda mrefu, kwa namna moja au nyingine ndiyo imekuwa inaibeba Wizara hii. Mheshimiwa Waziri anapotoa matamko ya mihemko ya haraka haraka anai-disturb industry. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri anaposema anafuta hizi leseni, naomba nimshauri, kwa sababu kuna vitalu 61 ambavyo havina watu. Kama angetaka vifanyiwe minada anayoitaka, angeanza na hivyo vitalu ambavyo havina watu mpaka sasa huko maporini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tasnia hii uwekezaji wake ni mkubwa sana. Anataka wakafanyie vitalu ambavyo wawekezaji wameweka pesa nyingi sana katika vile vitalu. Miaka mitatu ilioyopita, miaka mitano watu wamewekeza, wengine wamelea simba, halafu unasema wakafanye minada! Ni kuvuruga hii industry. Namshauri Mheshimiwa Waziri, hii tasnia inatakiwa achukue muda kui-study. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, binafsi nimefanikiwa kwenda katika maeneo mengi ambayo nimeona wame-invest hao wawekezaji. Kwa hiyo, tukianza ku-disturb kwa mihemko haitatusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashauri hawa Mawaziri vijana, fursa au opportunity is attracted by talent skill performance and ability. Show your talent and ability, people will love you. Be humble! Hao Mawaziri wa zamani kwa mfano, akina Lukuvi na Tizeba, tunawaona; wakijibu hoja, wanajibu hoja siyo za kimihemko. Unaridhika hata Mheshimiwa Waziri akikujibu, unapenda. Vijana wengi mnaonekana kama mnataka kufanya Serikali hii kiasi kwamba Serikali inayokuja mtakuwa hamna use. Kwa sababu mna mihemko sana. Onesheni ability na performance mnapofanya kazi zetu ili tuitunze Serikali...


T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S.MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tukiilaumu Serikali kwamba inaonekana kila mtu anafanya kivyake, hamja-synchronize. Wakati natoa hotuba yangu ya mambo ya nchi za nje mwaka 2017 nilizungumza, naomba ninukuu mahali nilisemaje?

Nilisema diplomasia ya uchumi pamoja na mambo mengine inahusu kuvutia fursa za wawekezaji wa kigeni (foreign investment), utalii (tourism) na biashara huria (free trade) kwa kufanya ushawishi wenye kufungua masoko mapya ya kuuza bidhaa za Kitanzania kupunguza au kuondoa masharti ya kodi na kusaidia wafanyabiashara na wawekezaji wa Kitanzania kuzitumia kikamilifu fursa za kiuchumi zinazopatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii tasnia; utalii huu umejengwa kwa muda mrefu sana. Akitokea mtu mmoja anaamua kufanya tu kwa kutaka cheap popularity atauvuruga kwa muda mfupi sana. Utalii unaingiza GDP kwa asilimia 20 na forex kubwa inatokana na utalii. Kwa hiyo, hicho siyo kitu kimoja ambacho mtu anaweza akaamka leo akasema nimeharibu. Hii diplomasia ya kiuchumi inategemea sana na kutabirika. Wawekezaji wanataka waone kwamba kunatabirika, tukienda tutafanya biashara zetu. Haiwezekani huyu Waziri, huyu huyu Waziri anatoa amri mpaka na mapolisi wanamkataa, anashindwa hata kuwasiliana na Waziri wake wa Mambo ya Ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu huyu Waziri anatoa amri, anapingana na Waziri wa Ardhi, huyo huyo mmoja! Huyu huyu Waziri anapingana na Waziri wa Uvuvi, huyu huyu Waziri mmoja. Hatuwezi kuwa na Mawaziri ambao wanafanya kazi kwa mizuka. Lazima wote kama

tunaliopenda Taifa letu tufanye kazi kwa kupendana na kuheshimiana katika mipaka. Ndiyo maana nimesema, kama Serikali hamja-synchronize kwamba vipaumbele vya nchi hii ni vipi? Kama vipaumbele hivi, tunataka tutekeleze diplomasia ya uchumi, maliasili ina-fit wapi? Foreign wako wapi? Uvuvi wako wapi? Tunataka tuuze wapi? Sasa kila mtu akiamka asubuhi ana mzuka wake, mara amebebe waandishi wa habari aondoke na makamera, akaseme anayoyataka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nimesema Waziri Mkuu anatakiwa awe hapa. Waziri wa Maliasili ndivyo tunavyomwona sisi kama Wabunge. Anai-disturb industry. Full time yuko kwenye twitter, kila wakati, utadhania Trump! (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ambayo nilisema ambayo nasema kama Serikali hamja-synchronize, nilisema Tanzania haina ajenda ya Taifa juu ya diplomasia ya uchumi wala mipango mikakati inayopimika (strategic plans) ambayo inabeba vipaumbele mahususi yaani specific priority. Tungekuwa na vipaumbele na mipango, maana yake tunge- synchronize. Waziri wa Maliasili anapoona mambo yake ya kiuchumi kuhusu wawekezaji lazima ashirikiane na Waziri wa Ardhi, atashirikiana na Waziri wa Kilimo, atashirikiana na Waziri wa Mifugo, lakini Waziri amekuwa na mihemko, anafanya mambo yake peke yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe ndugu zangu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)