Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuunga mkono mapendekezo ya Kamati hii, naomba kusisitiza kwamba migogoro ya ardhi hasa vijijini imezidi kuongezeka siku hadi siku. Kutopimwa ardhi kumesababisha miingiliano na vurugu kubwa hasa ikizingatiwa kwamba maeneo mengi ya vijijini hayajapangiwa matumizi bora ya ardhi zao, kwa mfano, Jimboni kwangu Same Mashariki, wakulima na wafugaji na TANAPA (Mkomazi National Park).
Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa wanyamapori kuingia kwenye mashamba na makazi ya wananchi umeongeza umaskini Jimboni kwangu. Mazao ya wakulima yamekuwa yakiharibiwa sana na wanyamapori. Wananchi wengine wameumizwa na wanyama hao. Badala ya kulipwa fidia, wananchi wamekuwa wakipewa kifuta jasho ambacho sio sawa na madhara waliyopata. Wanyamapori wamekuwa wakithaminiwa kuliko wananchi. Matokeo yake wananchi hawaoni faida ya kuwa na mbuga za wanyama katika maeneo yao. Nashauri Wizara hii ya Maliasili na Utalii ikishirikiana na Wizara ya Ardhi iweke utaratibu mzuri utakaoondoa matatizo haya ya wananchi.