Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kwa kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati pamoja na Kamati nzima kwa kazi nzuri ambayo tumeifanya kama Kamati, lakini kwa usimamizi mzuri wa Mwenyekiti wa Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ukurasa wa kwanza kwenye kitabu chetu, Kamati katika aya ya tatu imesikitishwa kwa kitendo cha kupigwa risasi Mbunge mwenzetu Mheshimiwa Tundu Lissu. Jambo hili lilisikitisha, lilistua, vilevile nimeshtuka sana wakati Wabunge wengine wakipongeza kitendo cha Kamati kusikitishwa na jambo hili niliona Wabunge wengine wamenuna, isipokuwa tu walipotajwa Wanajeshi 15 ndiyo watu wakapiga makofi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwangu binafsi imenisikitisha sana, ubaguzi wa wazi. Mbunge mwenzetu ameumizwa watu wamekaa kimya, hili jambo hatupaswi kulifumbia macho. Kwa sababu ya muda mdogo wengine watalizungumza, lakini hili ni jambo baya sana. Ninaiomba Serikali, sasa ni zaidi ya miezi mitano hakuna suspect hata mmoja! Tumeomba Vyombo vya Kimataifa vitusaidie kuwapata hao watu, Serikali inakataa. Ni lini Serikali itatuambia kuhusu tatizo hili ambalo lilifanyika mbele ya macho ya watu juu ya mwenzetu aliyepigwa risasi. Hili ni jambo la aibu na hatupaswi kulifumbia macho katika Taifa letu, ni jambo la hovyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, Mheshimiwa Heche juzi alizungumza hapa, mimi ni Mjumbe wa Kamati hii ambayo tunachangia, kuhusiana na suala e-passport ambalo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mwigulu alizungumza kwamba kilichozinduliwa siku ile ni e- immigration. Nataka nipate majibu halisi kwamba siku ile Mheshimiwa Rais alizindua e-immigration au ni e-passport?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima tujue jambo hilo kiundani. Kwa sababu Serikali hii imekuwa ikijipambanua kwamba ni Serikali inayokomesha ufisadi, lakini kiundani kama Kambi ya Upinzani tunazo nyaraka za kutosha, ambazo tutaziweka wakati muafaka. Nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka juu ya ufisadi na harufu kubwa ya ufisadi ndani ya jambo hili katika Serikali hii ambayo inayojipambanua kwamba ni Serikali inayopingana na ufisadi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano; katika mkataba ambao waliingia kwenye Memorandum of Understanding, bei ya passport moja ilikuwa inagharimu Pound za Uingereza 6.84, lakini hii e-passport iliyozinduliwa inagharimu Dollar 68 na ndiyo maana bei ime-shoot kutoka Sh.50,000 mpaka Sh.150,000. Mkurugenzi anasema kwamba hii ni ya miaka 15 hata ya Sh.50,000 tuliyokuwa tunatoa ilikuwa ni ya miaka 15 anyway. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, wananchi wa Watanzania hebu tuione hii Serikali inayojipambanua inakomesha ufisadi wakati kuna harufu kubwa na kwa kichaka cha Usalama wa Taifa. Pia niseme haya mambo ya kusema hela inayoenda Usalama wa Taifa Wabunge tusijue, hiyo siyo kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, tufuatilie nchi kama Israel, tufuatilie nchi kama Uingereza, Bunge tunayo haki ya kujua hela inayokwenda Usalama wa Taifa, isipokuwa hatuna haki ya kujua wanafanyaje ndani ya Usalama wa Taifa. Hata hivyo, kutudanganya kwamba tusijue hela inayokwenda Usalama wa Taifa ndiyo wizi unakopigiwa huko kwa kigezo cha kwamba haya ni mambo ya siri, masuala ya passport siyo mambo ya siri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na watu waliopewa kazi Memorandum of Understanding ni kwa nini walitolewa akaja akapewa mtu mwingine kinyemela nyemela? Hii ni hoja ya Mheshimiwa Heche….

T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ukicheza na nguruwe kwenye matope mtachafuka wote, lakini nguruwe atachekelea. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka nilizungumze …

T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili nataka nizungumze Polisi wamekuwa wakisema kwamba tutii sheria bila shuruti, lakini Polisi ndiyo wa kwanza wenyewe kuvunja sheria. Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, inamtaka Polisi akimkamata Mtuhumiwa ampeleke Mahakamani ndani ya masaa 24, lakini mimi ni shahidi nimekuwa mhanga wa kuingia mara nyingi Kituo cha Polisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, I am not criminal, I am a Politician, lakini kuna watu ambao wameomba niwasemee na Mheshimiwa Waziri unasikia hapa, wamekaa ndani ya Kituo cha Polisi kwa mfano Iringa Mjini, kabla ya Christmas miezi miwili wako ndani, hawatoi maelezo, hawapelekwi Mahakamani. Kwa nini tunawatesa watu?

Mheshimiwa Naibu Spika, mmezungumza hapa asubuhi nimeuliza swali la kupiga watu, Polisi wanapiga watu wanawavunja mpaka miguu, wanawaonea! Anakamatwa mtu hana makosa, amekamatwa mzima akifika ndani ya Kituo cha Polisi anapigwa, akipelekwa hospitali wanawaambia wasiwaandikie hata matibabu. Hii nchi tunaipeleka wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, wengine humu ndani tunapozungumza masuala ya Polisi mnaona kama vile hakuwahusu, wengine hata hamna legitimacy ya kuongea masuala ya Polisi. Kwa sababu you have never been there, hujawahi kwenda Magereza, hujawahi kwenda Polisi, unajaribu kuchangia, unadhani labda hakukuhusu! Hata kina Mramba walidhani hakuwahusu, lakini siku moja walienda.

Mheshimiwa Naibu Spika, mazingira ya kule ndani ni ya hovyo, Mbunge ambaye sina makosa nimechaguliwa na wananchi, natimiza majukumu yangu ya Kibunge …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji).