Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua anazochukua kukabiliana na Upotevu wa Mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua anazochukua kukabiliana na Upotevu wa Mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata fursa hii. Kwa kuwa Azimio limejikita katika kumpongeza Mheshimiwa Rais kutokana na tukio ambalo limetokea na sote tunampongeza kama ilivyofanya hotuba ya Mwenyekiti hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, CCM miaka yote tokea mwaka 1992 ni chama kipevu sana tokea huko nyuma kwa hiyo kilijiwekea miongozo ya kwamba kujikosoa leo kuliko jana na CCM imepanga lazima rasilimali za nchi ziwafaidishe wananchi. Katika kufikia lengo hilo ndiyo maana tukaona kwamba Marais wetu ambao wamepita wote walikuwa wana ripoti zao, Mheshimiwa Mkapa alikuwa ana ripoti, Mheshimiwa Mwinyi alikuwa ana ripoti, Mheshimiwa Dokta Kikwete alikuwa ana ripoti kuhusiana na suala hili la kufaidika na rasilimali za nchi. Hata hivyo, isitoshe tunafanya hivyo kwa lengo la kwamba ni lazima kuweka uwiano mzuri kati ya maslahi ya Taifa kwa wananchi wote pamoja na kuwavutia wawekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika pongezi zangu kwamba Rais Magufuli amejipambanua kutokana na wengine wote ingawaje kwamba wametokezea watu sasa wanajipaka damu za simba kama wao ndiyo walioua simba lakini simba tayari ameshauliwa sasa wanajitokeza. Hoja hii hata kama kuzungumzwa ilikuwa ikizungumzwa mpaka kwenye vibaraza vya kahawa kwamba vipi watu watafaidika na mchanga au na madini ambayo yapo katika nchi kwa hiyo siyo kwamba ni suala la fulani na fulani. Mimi naeleza hili kwamba Rais Dokta John Pombe Magufuli ni kiumbe na roho yake hawa wengine wote wanaojipakapaka ni midoli tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, katika Azimio hili tuiombe Serikali kwa upande wake iweze kupitia mikataba na kubaini mianya yote na kuiziba ili rasilimali za Taifa zisaidie Taifa. Pia kwa upande wa Bunge kama ilivyopendekezwa kwamba Serikali italeta marekebisho ya sheria, kwa hiyo, yatakapoletwa marekebisho ya sheria tuweze kuziba mianya yote, sisi ni Watanzania tuzilinde rasilimali zetu. Pamoja na hayo Waziri naye atengeneze taratibu kwa sababu madini haya yanatoka sehemu tofauti tofauti, kwa hiyo, hizo taratibu atakazoziweka ziwe sambamba na maeneo ambayo madini yetu haya yanatoka.